Malezi Duni na Utandawazi ndio Chanzo cha ongezeko la mijadala ya kupinga na kukosoa ndoa na maisha ya ndoa

Malezi Duni na Utandawazi ndio Chanzo cha ongezeko la mijadala ya kupinga na kukosoa ndoa na maisha ya ndoa

Kwa hyo hao wazazi wako walishushwa mbiguni ..Haukuzaliwa kuja kumtumikia mzazi wako inawezekana hata wazazi wako hawajwahi kusaidia wazazi wao.

Tengeneza familia yako na mwanamke mweny heshima wako kibao we endelea kufauta hawa sijui mmekutana chuo ,sijui mweupe

Acha kupangia watu maisha,wacha watu waishi wapendavyo.
 
Good morning Tanganyika!

Nimeshindwa kuvumilia baada ya kuona ongezeko la mada za kupinga kuoa, ndoa na maisha ya ndoa! Jamii Forum ni kama kioo cha Taifa kwasasa. Think tank kubwa ya nchi nathubutu kusema iko humu JF, sasa kitu kinapotrend sana Jamii forum ni lazima upate picha ya kinachoendelea nchini.

Hili ongezeko la mada za kupinga, kukosoa, kukejeli ndoa na maisha ya ndoa si jambo zuri hata kidogo bali ni msiba kwa taifa zima! Kuna sumu mbaya wamelishwa vijana wetu na imewaingia barabara!
~ Kukataa ndoa ni kukataa kujikubali.
~ Ni kukataa kujitambua.
~ Ni kukataa majukumu.
~ Ni kukosa malezi sahihi.
~ Ni kukosa akili.
~ Ni kukosa hekima.
~ Ni kwenda kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu (kwa waamini).
~ Ni kukosa upendo upeo na maono!

Tunataka kuunda Taifa gani bila ndoa?
~ Ndoa ndio chanzo cha familia.
~ Ndoa ni dalili njema ya ukomavu wa akili.
~ Ndoa ni msingi wa uwajibikaji kujali, amani, furaha na upendo.
~ Ndoa ni future, bila ndoa future haina maana sana.

~ Makuzi yasiyo sahihi.
~ Wazazi wasiojitambua.
~ Wazazi wasio na muda wala ukaribu na familia zao.
~ Utandawazi.
~ Elimu potofu mitandaoni juu ya dhana nzima ya ndoa na maisha yake ni visababishi vikubwa mno vya matokeo hasi wanayopata vijana kuhusu ndoa na wao bila kujitambua huyafanya hayo kama ndio uhalisia na kuja na mada za kila aina.

Kama maandiko ya misahafu ya kiimani yanawaasa wanaume waishi na wanawake kwa akili, tafsiri yake ni kwamba mkataa ndoa hana akili ndio maana hawezi kuishi maisha ya ndoa.

Ukomavu wa kiakili, maono na hekima hukufanya uitamani ndoa ili kujipima. Uwezo wako wa kumudu maisha ya ndoa. Utayari wako wa kuhudumia ndoa. Ujasiri wako wa kuyakabili magumu ya ndoa nk, nk.

Ndoa ni kwa ajili ya wanaume kamili. Ndoa si kwa ajili ya wavulana!

Mjadala utaendelea.

Wanao kataa ndoa wana hoja zao za msingi wasikilizwe,halafu tangu lini binadamu wote tukawa sawa.
 
Wanaokomalia hii kampeni wengi ndo hao hao wanaofanya kampeni ya mapenzi ya jinsia moja., na wengine ni kukwepa majukumu.
Hatukatai kwamba ndoa zina matatizo mengi tu lakini haimaanishi ya kwamba kila ndoa ina matatizo, wapo wanaoishi vizuri bila tatizo.
Na wanaposema tukatae ndoa ina maana watu waache kuzaliana? Au ndo wanafurahia ongezeka la single mothers?


Sent from my LM-V500N using JamiiForums mobile app
 
Hata wwe unaelekea kuwa mzazi amini ..Tafuta familia ,tabia usizozipenda usivumilie kabisa kwa mkeo mtarajiwa Bora ukachukue kijijini.

Angalia tabia za mama ako na jinsi alivyokulea basi nawe tafuta mwanamke mwenye tabia izo ikiwezekana muombe mama ako akutafutie mchumba kutoka jamii yake.

Hapa kwenye Mama kutafuta mchumba kuna point ingawa vijana wa kike na kiume wanaweza wasielewe kirahisi
 
mshana umelaumu sana upande mmoja bila kutuwekea sababu zao, ingependeza utuwekee sababu zao tuzipime, ili tujue, vipi hao unaotaka waolewe, wao wanajitambua? wana malezi bora toka kwa wazazi wao? wana akili? wana hekima? wana upendo, upeo, na maono?

Mimi nadhani anashauri wale wanaojitambua kwa pande zote mbili, waoaji na waolewaji…..

Faida za kuoa alizotoa ni muda mrefu na faida za kutokuoa nyingi unaona zinaishia ujanani, anyway kila munu na lwake
 
Ukiona mwanamke anachepuka kisababishi kwa asilimia 90 ni mwanaume nina mifano ya kutosha
Mshana Jr hii ni Feminine Ideology. kama Mwanaume hutakiwi kuzungumza kauli ya namna hio unapowashauri Vijana. Weka Mzani sawa ili kila mtu ajue wajibu wake anapoingia huko kwenye NDOA.

Kuchepuka 99% ni tabia na maamuzi ya Mtu, hakuna Bahati mbaya wala kusababishiwa. hizo ni Excuse tu. Uchepukaji ni Maamuzi ya mtu husika. Kisababishi ni yeye mwenyewe.

Kwenye hiyo Mifano yako ya kutosha naomba hata Mitatu utuonyeshe namna Mwanaume anasababisha Mwanamke kuchepuka. May be definition ya kuchepuka tunatofautiana.
 
Kizazi kilichokengeuka, wanaume vichwa vipo race kama gari ya langalanga wanawake nao madishi yameyumba kama yamepigwa na cyclone.

Hiyo ndoa hata ikifungwa ndani ya miezi kadhaa walishaachana.

Ndio maana wanaona haina haja ya kuoa.
Kweli kabisa kwanini vichaa wawili waoane? Wataishia kuuana, tuwaache waishi hivyo hivyo. Ila tuwaombe kwa msisitizo mkubwa sana wajitahidi kulea vizuri watoto wanaowapata huko kwenye uzinzi, Jamii inaharibika zaidi panapokua na malezi ambayo hayana utaratibu maalumu.
 
Back
Top Bottom