Mbwa dume
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 5,934
- 10,206
Kaka Mshana Jr ulichoongea ni sahihi lakini angalia asilimia kubwa ya wanawake wa sasa ni pasua kichwa yaani ni wale wa haki sawa ukikohoa naye anakohoa!Good morning Tanganyika!
Nimeshindwa kuvumilia baada ya kuona ongezeko la mada za kupinga kuoa, ndoa na maisha ya ndoa! Jamii Forums ni kama kioo cha Taifa kwasasa. Think tank kubwa ya nchi nathubutu kusema iko humu JF, sasa kitu kinapotrend sana Jamii forums ni lazima upate picha ya kinachoendelea nchini.
Hili ongezeko la mada za kupinga, kukosoa, kukejeli ndoa na maisha ya ndoa si jambo zuri hata kidogo bali ni msiba kwa taifa zima! Kuna sumu mbaya wamelishwa vijana wetu na imewaingia barabara!
~ Kukataa ndoa ni kukataa kujikubali.
~ Ni kukataa kujitambua.
~ Ni kukataa majukumu.
~ Ni kukosa malezi sahihi.
~ Ni kukosa akili.
~ Ni kukosa hekima.
~ Ni kwenda kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu (kwa waamini).
~ Ni kukosa upendo upeo na maono!
Tunataka kuunda Taifa gani bila ndoa?
~ Ndoa ndio chanzo cha familia.
~ Ndoa ni dalili njema ya ukomavu wa akili.
~ Ndoa ni msingi wa uwajibikaji kujali, amani, furaha na upendo.
~ Ndoa ni future, bila ndoa future haina maana sana.
~ Makuzi yasiyo sahihi.
~ Wazazi wasiojitambua.
~ Wazazi wasio na muda wala ukaribu na familia zao.
~ Utandawazi.
~ Elimu potofu mitandaoni juu ya dhana nzima ya ndoa na maisha yake ni visababishi vikubwa mno vya matokeo hasi wanayopata vijana kuhusu ndoa na wao bila kujitambua huyafanya hayo kama ndio uhalisia na kuja na mada za kila aina.
Kama maandiko ya misahafu ya kiimani yanawaasa wanaume waishi na wanawake kwa akili, tafsiri yake ni kwamba mkataa ndoa hana akili ndio maana hawezi kuishi maisha ya ndoa.
Ukomavu wa kiakili, maono na hekima hukufanya uitamani ndoa ili kujipima. Uwezo wako wa kumudu maisha ya ndoa. Utayari wako wa kuhudumia ndoa. Ujasiri wako wa kuyakabili magumu ya ndoa nk, nk.
Ndoa ni kwa ajili ya wanaume kamili. Ndoa si kwa ajili ya wavulana!
Mjadala utaendelea.
Wanawake wamefikia mahala anakupangia zamu ya kufua, kupika, kupewa mbususu tena ukute hawa wasomi halafu awe na kiajira ndo utaisoma namba maana atakwambia yuko busy na majukumu ya kiserikali hana muda wa kumjali mmewe ukiomba mbususu unasukumwa kule eti amechoka!
Mwanamke wa siku hizi anaweza kumfokea mumewe mbele ya watoto na ukimjibu anafungulia bomba la maneno ya shombo mpaka utajuta!
Zamani hakukuwa na kesi za mme kumzaba makofi mkewe ila leo hii hata ukimsema tu mkeo anaenda kushtaki na unakuja kukamatwa.
Mbaya zaidi siku hizi wake za watu ndo wanaongoza kwa kuuza mbususu bila hata uoga iwe maofisini, hawa mama wa nyumbani ndo usiseme kabisa!
Maisha yenyewe stress halafu mke naye akupe stress utakimbilia wapi?
Mimi binafsi nimeoa(japo sio kivile sana)
Lakini simshauri kijana kuoa tena kama hajawa na maisha ya kueleweka (kipato)
Maana kwa maisha ya sasa faida na raha ya ndoa ni kidogo sana ukilinganisha na hasara za kuoa!
Huo ni mtazamo wangu acha nilog off nikafungue banda langu la majeneza nisubiri wateja maana hizi tarehe mambo si haba.