Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
- Thread starter
- #121
ASIWAJU kwa mtazamo wa haraka hakuna tatizo kabisa mtu asipooa au kuolewa.. Lakini huu ni mtazamo wa ujanani unapokuwa damu inachemka na una nguvu ya kufanya karibu kila kitu mwenyewe na huna changamoto yoyote ya maisha1. Kwani kuna tatizo/madhara mtu asipo oa au olewa ?
2. Kwani ndoa ni swala la lazima au hiari ?
3. Umuhimu wa ndoa upo wapi ambao hawaja oa wana ukosa ?
Naomba mleta mada unipatie majawabu ya hayo maswali matatu ya mwanzo.
Swali la pili ndoa si suala la lazima au hiari bali ni uamuzi binafsi
Umuhimu wa ndoa huonekana nyakati za shida kubwa, upweke changamoto za kimaisha, magonjwa na uzee.. Kuna mahali unafika unahitaji wa kukuhudumia na kukusaidia maana hujiwezi tena! Huyo hawezi kuwa mzazi ndugu, mtoto ama rafiki
Kuna nyakati unamhitaji mtu wa kukaa naye na kumweleza hisia zako, maumivu yako furaha yako maono yako nk
Katikati ya hali zote hizi na nyinginezo mtu huyo si mwingine bali ni mke au mume