Malezi Duni na Utandawazi ndio Chanzo cha ongezeko la mijadala ya kupinga na kukosoa ndoa na maisha ya ndoa

Malezi Duni na Utandawazi ndio Chanzo cha ongezeko la mijadala ya kupinga na kukosoa ndoa na maisha ya ndoa

Aidha binafsi uwe na kitu na mwanamke awe na kitu ndio muungane hakuna kupeana lift, na mali ya kila mmoja itambulike hapo ndipo upendo wa kweli utajidhihirisha.
Kila siku huwa nasema wanawake HAWANA UPENDO WA KWELI KABISA zaidi ya kinyemela fedha zako, ngoja zikuishie ndipo utajua mpendwa alikuwa ni fedha na si wewe, pumbavu sana.
Hakuna mwanamke nimekutana nae ambaye anatoa mali yake au pesa zake kwa moyo mkunjufu kabisa bila kuiwaza na kuikumbuka kila saa na kuanza kutengeneza mazingira ya kuidai.

Kimsingi mwanamke anawaza kupata sio kutoa, na anatoa pale ambapo atapata zaidi ya anachotoa zaidi.
 
Hahaha mkuu hivi siyo ninyi ambao mkiajiri housegirls baadaye mnaanza kulalamika kuwa oo sijui mke kajisahau sana housegirl ndio anafanya kila kitu na mwisho mnaanza kutembea na hao housegirls

Sent from my S6 using JamiiForums mobile app
Mimi mke wangu hata asipogusa chochote kama housegirl yupo na kufanya kazi yake vizuri, nitampongeza mke wangu kwa kusimamia vizuri huyo housegirl.
Mwanaume ni kichwa cha familia mwanamke ni mwili..
Mwanaume (Kichwa) hufikiria, kuweka mipango na kutafuta njia..
Bila mwanamke (mwili) thabiti kufikia ndoto na malengo ni ngumu..
Nyumbani kunavyumba siingii hata mwezi , fridge sifungui ,sijui watoto wanavaa nini ,ratiba ya chakula, nyumba imefanyiwa usafi au vipi .Hata akiwa anauwezo wa kuviweka vizuri aweze kusimamia zoezi zima
Zaidi anitii aniheshimu, anipe moyo ninapo chafukwa, aniamini (kama kunasehemu sijaridhika nitatoa ushauri nasiyo kulazimisha, kwasababu hilo ni eneo lake)

Kazi yangu kubwa kama (kichwa) Kumpenda na kumuonyesha kwa matendo, kuhakikisha na invest wapi penye return nzuri, najenga misingi gani kwaajili ya baadae, natengeneza connection gani zitakazo kusaidia kizazi changu , bajet ya matumizi ya familia naimudu, kumpa nafasi ,kumsikiliza mke wangu na ushauri wake, kumpa muda mke wangu na familia na kutokuendekeza marafiki wasio na maana wala kuongeza kitu chanya kwenye maisha yangu. (kama kunasehemu hajaridhika atatoa ushauri nasiyo kulazimisha maana ni eneo langu).
 
Mkuu kukataa ndoa sio kukataa kuishi na mwanamke , kinacho pigwa apa ni kufunga pingu za maisha .
Sawaaa....lakini kama hamjafunga ndoa nani atakuwa msimamizi wa malinza watoto ukiwa haupo??
Kaka?, Dada?, Mjomba?
Watoto wako watakuwa hawana chao na mama atakuwa hana nguvu ya kuwapambania.
Tuangalie mbali zaidi ya tamaa zetu
 
Sasa ulitaka mwanamke ndo akuhudumie wewe? Na majukumu ya kubeba mimba utabeba wewe sio? Ovyo kabisa ndomana mnaolewa na wanaume wenzenu sababu ya kupenda mseleleko pole kwa mama yako ya baba yako.
Issue sio kuhudumia. Issue ni unahudumia mtu wa aina gani. Mabinti wa sasa mpo so focused kwenye kuhudumiwa ila mkiulizwa mnajua majukumu yenu katika mahusiano tukianza na lile la kutii na kuheshimu unakuta ni zero hakuna mnachofahamu.

Kimsingi, gari bovu lina gharama kubwa sana kulimiliki na kulitunza. Ni ujinga sana kufocus kuwa m'miliki wa gari badala ya kufocus na aina gani ya gari unataka kumiliki na namna utaweza ukimudu.

Mwanamke ambaye hajakuzwa vema kuwa mke na mama bora ni wa kazi gani kwa mwanaume?!

Wengi mnachohisi ni cha thamani mnachowapa wanaume ni hapo kati basi hakuna la ziada.
 
ASIWAJU kwa mtazamo wa haraka hakuna tatizo kabisa mtu asipooa au kuolewa.. Lakini huu ni mtazamo wa ujanani unapokuwa damu inachemka na una nguvu ya kufanya karibu kila kitu mwenyewe na huna changamoto yoyote ya maisha

Swali la pili ndoa si suala la lazima au hiari bali ni uamuzi binafsi

Umuhimu wa ndoa huonekana nyakati za shida kubwa, upweke changamoto za kimaisha, magonjwa na uzee.. Kuna mahali unafika unahitaji wa kukuhudumia na kukusaidia maana hujiwezi tena! Huyo hawezi kuwa mzazi ndugu, mtoto ama rafiki
Kuna nyakati unamhitaji mtu wa kukaa naye na kumweleza hisia zako, maumivu yako furaha yako maono yako nk
Katikati ya hali zote hizi na nyinginezo mtu huyo si mwingine bali ni mke au mume
Me naona Mshana Jr unakwepa hoja ya msingi hapa kwenye huu mjadala. Si kwamba watu wanapinga ndoa ila hapa ukitazama upande wetu sisi wanaume kuna vitu tunazungumzia hapa na wanawake wanavideflect kama sio kuvikwepa kujibu ile direct.

Kwa kifupi wanawake wanakwepa kuwajibika kwa matendo yao ambayo ndiyo kichochezi cha mdororo wa ndoa.

Sababu hizo ni kama tabia mbovu, umalaya, kiburi, kuwa na watoto kabla ya mahusiano serious, kuweka mbele masilahi yao binafsi wakitegemea kuchuma kwa mwanaume na kuweka kando.


Haya mbona kama yanakwepwa?!
 
Basi ndio mkubali kwamba mke akiwa mfanyakazi au mfanyabiashara hataweza kutimiza majukumu ya nyumbani ikiwemo na kukulea wewe pamoja na watoto ipasavyo hivyo muache kulala

Basi ndio mkubali kwamba mke akiwa mfanyakazi au mfanyabiashara hataweza kutimiza majukumu ya nyumbani ikiwemo na kukulea wewe pamoja na watoto ipasavyo hivyo muache kulalamika
Kwa upande wangu nimekubaliana nalo kabisa kwasababu akili yangu nimeiweka kwamba yotehayo anafanya kwa maendeleo yetu hata kama ni kidogo anachochangia kwakungu inaonesha ni jinsi gani anajitoa siyo kwa maneno tu bali kwa vitendo kwangu mimi, watoto na ndoa yake.
Kuna vitu huwezi kununua mkuu, utanunua tendo la ndoa na uta mlipa mtu wa kutunza njumba na watoto wako tena vizuri.
Lakini huwezi nunua mke bora anaye jitoa kwaajili ya ndoa yake, mume wake na watoto wake kwanguvu na akili zake.....
 
Usiwaone wajinga Wana hoja

Labda km na wewe huna mke hujui..Stress za kijinga wanazopitia wanaume ..

Hawa ndugu zetu kwa sasa ni kama they have nothing to offer zaidi ya stress....

Ishu hapa sio kukataa ndo ishu ni wanawake wakuoa hamna..

Mi nina mke lakini hata Leo hii akisema anaondoka sijioni km nimepoteza kitu cha msingi maishani yaani kwanza sijioni kama nitapungukiwa kitu..

Yaani ukikaa chini ukasema hivi huyu ana msaada gani specific kwenye Maisha yangu kiujumlA sioni labda ile tu Ana mke huyu, jamaa Kaoa basiiiiiii..

In fact, nilivyokuwa bachela ndo nilikuwa na enjoy maisha zaidi kuliko nilivyooa..

Wanawake hawana Cha kutoa huu ndo ukweli mchungu ila tutaona km biblia inadanganya.Maana iliandika ipo siku wanawake watalazimisha Ndoa watakuja Kumi kumi ila watakosa mume..

Madogo ni KWELI,msikimbilie Ndoa.Wengi wenu huko ndo mtaenda kuharibu maisha yenu..

Ndoa Ina mtaka mwanaume ajitoe kwa Kila kitu wakati mwanamke hana Cha kutoa..mpumbavu tu na asiye na mke ndo atasema wasiooa wajinga..

Kuoa ni kubahatisha mwenye bahati tu ndo atapata mke bora..Jiulize una bahati????

Kuna mtu rahisi ku mplease km mwanaume??? vitu basics tu chakula kitamu ,uchi, heshima ila 75% hawapati hivyo vitatu.
 
Hata wwe unaelekea kuwa mzazi amini ..Tafuta familia ,tabia usizozipenda usivumilie kabisa kwa mkeo mtarajiwa Bora ukachukue kijijini.

Angalia tabia za mama ako na jinsi alivyokulea basi nawe tafuta mwanamke mwenye tabia izo ikiwezekana muombe mama ako akutafutie mchumba kutoka jamii yake.
Hili ni gumu sana kwa sasa..Wazazi hawaishi sana na watoto kama ilivyokuwa huko zamani .Kwahiyo anaweza kuwa na mtoto lakini asimfahamu tabia yake ya kweli akiwa nyumbani na maeneo ya nyumbani ana act tu
 
Good morning Tanganyika!

Nimeshindwa kuvumilia baada ya kuona ongezeko la mada za kupinga kuoa, ndoa na maisha ya ndoa! Jamii Forums ni kama kioo cha Taifa kwasasa. Think tank kubwa ya nchi nathubutu kusema iko humu JF, sasa kitu kinapotrend sana Jamii forums ni lazima upate picha ya kinachoendelea nchini.

Hili ongezeko la mada za kupinga, kukosoa, kukejeli ndoa na maisha ya ndoa si jambo zuri hata kidogo bali ni msiba kwa taifa zima! Kuna sumu mbaya wamelishwa vijana wetu na imewaingia barabara!
~ Kukataa ndoa ni kukataa kujikubali.
~ Ni kukataa kujitambua.
~ Ni kukataa majukumu.
~ Ni kukosa malezi sahihi.
~ Ni kukosa akili.
~ Ni kukosa hekima.
~ Ni kwenda kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu (kwa waamini).
~ Ni kukosa upendo upeo na maono!

Tunataka kuunda Taifa gani bila ndoa?
~ Ndoa ndio chanzo cha familia.
~ Ndoa ni dalili njema ya ukomavu wa akili.
~ Ndoa ni msingi wa uwajibikaji kujali, amani, furaha na upendo.
~ Ndoa ni future, bila ndoa future haina maana sana.

~ Makuzi yasiyo sahihi.
~ Wazazi wasiojitambua.
~ Wazazi wasio na muda wala ukaribu na familia zao.
~ Utandawazi.
~ Elimu potofu mitandaoni juu ya dhana nzima ya ndoa na maisha yake ni visababishi vikubwa mno vya matokeo hasi wanayopata vijana kuhusu ndoa na wao bila kujitambua huyafanya hayo kama ndio uhalisia na kuja na mada za kila aina.

Kama maandiko ya misahafu ya kiimani yanawaasa wanaume waishi na wanawake kwa akili, tafsiri yake ni kwamba mkataa ndoa hana akili ndio maana hawezi kuishi maisha ya ndoa.

Ukomavu wa kiakili, maono na hekima hukufanya uitamani ndoa ili kujipima. Uwezo wako wa kumudu maisha ya ndoa. Utayari wako wa kuhudumia ndoa. Ujasiri wako wa kuyakabili magumu ya ndoa nk, nk.

Ndoa ni kwa ajili ya wanaume kamili. Ndoa si kwa ajili ya wavulana!

Mjadala utaendelea.
STAMINA amesikia lakini....?
 
Hutaki wewe kaa kutulia,kwani watu wasipo oa wewe kinakuwasha nini?kila mtu na maisha yake.
Kama we ni msukuma isiwe sababu ya kunishawishi ugali n mtamu ..Pambana na ushamba wako ..Kila mtu ashinde mechi zake hauna jipya la kunifundisha
 
Naropoka haya kajambe.

Nyie ndo mnatengeneza watoto wa mitaani watoto wanaokosa malezi ya baba na mama. Unadhani malezi ya mtoto ni kumwaga tu mbegu na kwenda labor.
Watoto wa kiume wanazaliwa na kukosa malezi ya baba unajua madhara yake au una bwabwaja tu.

Kuoa ama kuolewa sio lazima, lakini kufanya kampeni ili kubadilisha mind ya kila mtu haikubaliki.
Unachoona hakikufai mwenzio kinamfaa.

Kaa hapo usioe, ukazae huko na uwaambie watoto wako wasije kuoa ama kuolewa.

Wewe unachokifanya hakina tofauti nao,nawewe una ajenda hiyo hiyo ya kulaziamisha watu wa owe,ndoa ni hasara kwa mwanamme na faida kwa mwanamke.
 
Good morning Tanganyika!

Nimeshindwa kuvumilia baada ya kuona ongezeko la mada za kupinga kuoa, ndoa na maisha ya ndoa! Jamii Forums ni kama kioo cha Taifa kwasasa. Think tank kubwa ya nchi nathubutu kusema iko humu JF, sasa kitu kinapotrend sana Jamii forums ni lazima upate picha ya kinachoendelea nchini.

Hili ongezeko la mada za kupinga, kukosoa, kukejeli ndoa na maisha ya ndoa si jambo zuri hata kidogo bali ni msiba kwa taifa zima! Kuna sumu mbaya wamelishwa vijana wetu na imewaingia barabara!
~ Kukataa ndoa ni kukataa kujikubali.
~ Ni kukataa kujitambua.
~ Ni kukataa majukumu.
~ Ni kukosa malezi sahihi.
~ Ni kukosa akili.
~ Ni kukosa hekima.
~ Ni kwenda kinyume na maagizo ya Mwenyezi Mungu (kwa waamini).
~ Ni kukosa upendo upeo na maono!

Tunataka kuunda Taifa gani bila ndoa?
~ Ndoa ndio chanzo cha familia.
~ Ndoa ni dalili njema ya ukomavu wa akili.
~ Ndoa ni msingi wa uwajibikaji kujali, amani, furaha na upendo.
~ Ndoa ni future, bila ndoa future haina maana sana.

~ Makuzi yasiyo sahihi.
~ Wazazi wasiojitambua.
~ Wazazi wasio na muda wala ukaribu na familia zao.
~ Utandawazi.
~ Elimu potofu mitandaoni juu ya dhana nzima ya ndoa na maisha yake ni visababishi vikubwa mno vya matokeo hasi wanayopata vijana kuhusu ndoa na wao bila kujitambua huyafanya hayo kama ndio uhalisia na kuja na mada za kila aina.

Kama maandiko ya misahafu ya kiimani yanawaasa wanaume waishi na wanawake kwa akili, tafsiri yake ni kwamba mkataa ndoa hana akili ndio maana hawezi kuishi maisha ya ndoa.

Ukomavu wa kiakili, maono na hekima hukufanya uitamani ndoa ili kujipima. Uwezo wako wa kumudu maisha ya ndoa. Utayari wako wa kuhudumia ndoa. Ujasiri wako wa kuyakabili magumu ya ndoa nk, nk.

Ndoa ni kwa ajili ya wanaume kamili. Ndoa si kwa ajili ya wavulana!

Mjadala utaendelea.
Tatizo Zinaa imekua rahisi sanaa na inazidi kurahisishwa kadri siku zinavoenda ndo mna mtu anaona ya nini kuoa kma kile ambacho angekipata ndani ya ndoa anakipata sasa

Ndo wale wanosema

Kwanini nifuge ng'ombe wakati maziwa napata

Ila kumbuka
#uzinzi haujawahi kumuacha mtu salama#
 
Back
Top Bottom