Lucas Julson
Member
- Sep 8, 2014
- 12
- 4
UTANGULIZI.
MALEZI ENDELEVU INITIATIVE (MEI) ni wazo la kuandaa mfumo kamili wa kumlea Mtoto wa kitanzania kabla ya kuzaliwa, kuzaliwa mpaka utu uzima ili kujenga Tanzania imara na endelevu.
MEI inalenga kumuandaa Mtoto katika nyaja mbalimbali kama;

- Kimwili
- Kiroho
- Kiakili
- Kiuchumi
- Kijamii
- Kihisia
- Kisaikolojia
MEI inaamini jamii inaundwa na mtu mmoja na hivyo akiwepo mtu mmoja mwenye utimamu katika nyaja tajwa hapo juu na akaungana na mtu mwingine mwenye utimamu basi jamii nzima itakuwa imara na endelevu.
Tumekuwa mashuhuda wa namna maadili yanavyoendelea kuporomoka na kila mtu, jamii, makundi mbalimbali na viongozi wanajaribu kuona na kushauri ni kwa namna gani kama taifa la Tanzania tunaweza kufanya ili kuijenga TANZANIA IMARA NA ENDELEVU.
View: https://youtu.be/pZBiHpLfdBo?feature=shared
View: https://youtu.be/PSaLjqsORm8?feature=shared
View: https://youtu.be/z9uWQ0HMNhI?feature=shared
Lakini pia tumekuwa mashuhuda wa changamoto mbalimbali ambazo hutokea mara kwa mara kwa Mama wajawazito kama vifo, kujifungua kwa upasuaji, pressure za mimba, Watoto njiti n.k
MALEZI ENDELEVU INITIATIVE - MZUNGUKO WA MALEZI.
MEI inaamini katika mzunguko wa Malezi kama ifuatavyo;
Alfa: Baada ya ndoa, kabla ujauzito ( Miaka T mpaka Miaka 0/miezi 0 )
Bravo: Kipindi cha ujauzito ( Miezi 0 mpaka Miezi 9 )
Charlie: Kipindi cha uchanga ( Chini ya miezi 6 mpaka Miaka 2 )
Delta: Kipindi cha Utoto ( Miaka 3 mpaka miaka 8 )
Echo: Kipindi cha chipukizi(teenager) (Miaka 9 mpaka Miaka 17)
Foxtrot: Kipindi cha Ujana (Miaka 18 mpaka Miaka T)
NB; T ni siku ya kufunga ndoa
Baada ya kipindi cha Ujana kinarudi kipindi cha Bravo, huu mzunguko wa Malezi unawahusu watu watatu yaani BABA, MAMA na MTOTO.
MEI inaamini Malezi ya Mtoto yaanza kabla ya kutungwa kwa mimba yake yaani Maisha ya MKE na MUME kwenye kipindi cha ALFA huamua Maisha ya Mke kipindi cha BRAVO na kuendelea mpaka Mtoto atakapofika utu uzima na kuwa Mzazi yaani kuwa BABA au MAMA. Kama kipindi cha ALFA kitaandaliwa vizuri na kwa kufuata kanuni zote za kitaalamu basi kipindi cha Ujauzito kitapita salama bila changamoto zozote na kipindi cha uchanga pia. Kama vipindi vyote hivi vitazingatia kanuni na taratibu zote basi Tanzania tutakuwa na jamii Imara na Endelevu (kiakili, kiroho, kimwili, kihisia, kiuchumi, kijamii, kisaikolojia) na hivyo kuwa Taifa Imara pia.
MEI inaamini Familia ndiyo sehemu pekee ya kuweza kutengeneza Taifa Bora, hivyo inaamini ikiwa Baba na Mama watapatiwa kanuni za kufuata kabla ya kupata mtoto wanaweza kupata Mtoto imara na timamu na hivyo kufanya jamii imara na baadaye Taifa bora.
Tujiulize swali, mfano watu wote wangetoweka Duniani na kusaliwa na watu wawili tu yaani Mke na Mume, na tunataka kuanzisha Jamii imara na endelevu; Je, watu hawa wawili wanatakiwa kuishi kwa namna gani ili kutokea kwao tupate jamii Imara na endelevu???
MEI imegawa Malezi katika Vipindi sita tofauti na kila kipindi kina matokeo Chanya au Hasi katika kipindi kingine yaani kipindi cha Alfa huamua Maisha yatakavyokuwa kwenye kipindi cha Bravo na kipindi cha Bravo huamua Maisha yatakavyokuwa kwenye kipindi cha Charlie na kuendelea.
MEI inaamini mahitaji katika vipindi hivyo ni tofauti yaani Mjamzito anatakiwa kupewa mahitaji maalumu kabla ya Ujauzito na baada ya mimba ili mtoto akue vizuri katika maeneo tuliyoyataja, Yaani maandalizi ya kupata Ujauzito, kipindi cha Mimba, kipindi cha Uchanga na kuendelea, Baba na Mama wana wajibu tofauti na kwa vipindi tofauti ili kuwa na matokeo Chanya.
MEI inaamini mtoto mpaka kufikia hatua ya Utu uzima ana mahitaji tofauti tofauti kulingana na kipindi alichopo yaani akiwa ndani ya tumbo, akizaliwa na kuendelea.
WADAU MUHIMU KATIKA KUTENGENEZA MFUMO WA MALEZI ENDELEVU INITIATIVE (MEI)
MEI inalenga kukutanisha wataalamu wabobezi wa maeneo yaliyoanishwa mwanzo ili kila mmoja aweze kutoa kanuni za namna bora ya kumlea mtoto na mama kuanzia kabla ya ujauzito mpaka utu uzima. Wataamu wafuatao MEI inalenga kukutanisha wataalamu wafuatao;

- Viongozi wa dini.
- Viongozi wa kimila.
- Wataalamu wa afya.
- Wataalamu wa Mazoezi ya viungo.
- Wataalamu wa Lishe.
- Wataalamu wa Saikolojia.
- Serikali kupitia Wizara husika.
- Wataalamu wa Elimu juu ya Maisha.
Hapa kila mtaalamu ataeleza namna na kanuni za kuzingatia kwa kufuata Vipindi husika yaani kabla ya ujauzito, baada ya mimba nani?, afanyiwe nini?, kwa nini?, na kwa namna gani?, na kwa wakati gani? ili kuleta matokeo chanya kiroho, kimwili, kiakili, kihisia n.k
UTEKELEZAJI WA MFUMO WA MALEZI ENDELEVU INITIATIVE (MEI)
Baada ya hapo MEI itaandaa mfumo kamili katika maandishi na baada ya hapo tutaingia katika utekelezaji kama ifuatavyo;

- Viongozi wa dini na watu wote wanaohusika kufungisha NDOA wahakikishe kabla ya vijana kufungishwa ndoa wawe wamefundishwa na kuelewa mfumo huu kwa vitendo na itungiwe sheria kabisa.
- Vituo vyote vya kulelea Watoto watumie mfumo huu katika kuwalea Watoto waliopo chini ya vituo hivyo.
- Vijana wanaomaliza shule ya sekondari wanapoenda Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wafundishwe kikamilifu na wawe imara katika mfumo huu.
- Kuwe na muendelezo wa kufundisha mfumo huu kwa Vijana kabla ya kutimiza miaka 18.
"Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (MMMAM) ni suala muhimu kwa maendeleo na ustawi wa Taifa. Suala hili linabeba huduma zote muhimu anazostahili kupewa mtoto mdogo miaka 0 hadi 8 ili kumwezesha kukua na kufikia utimilifu wake katika nyanja zote za kimwili, kiakili, kijamii, kihisia, kimaadili, kimaono, na baadaye kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa na kumwezesha kumudu mazingira yake. Ushirikiano wa wadau katika utoaji huduma jumuishi za MMMAM ndiyo njia pekee itakayowezesha watoto kukua na kufikia utimilifu wao." Chanzo kutoka "kiunzi cha malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto Tanzania" TECDEN 2013
MALEZI ENDELEVU, TAIFA ENDELEVU (SUSTAINABLE PARENTING, SUSTAINABLE NATION)
Upvote
5