Sema Tanzania
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 251
- 466
Iwapo unasafiri na mtoto mdogo mwenye umri chini ya kwenda shule. Uwapo katika daladala na mtoto umri huu hapaswi kulipiwa nauli. Mara nyingi husimama kati ya miguu yako ama pengine unampakata. Taratibu za LATRA zinasema huyu halipiwi nauli. Lakini kama unasafiri naye katika mabasi makubwa ya kwenda safari ndefu nje ya mji; mfano Dar es salaam hadi Mwanza au Mbeya hadi Dodoma, na iwapo atakalia kiti – basi utawajibika kumlipia nauli ya mtu mzima.
Mabasi makubwa ya safari ndefu. Ingawa utaratibu wa daladala mijini ni kuwa mwanafunzi atalipa nusu ya nauli ya mtu mzima, katika mabasi makubwa ya safari ndefu watoto wanafunzi na watu wazima wote nauli ni sawa. Maandalizi ya safari. Takwimu zinaonesha kwamba wasafiri wengi wa safari ndefu hulala wawapo safarini. Hivyo iwapo unapanga kusafiri na watoto wako, jipe muda wa kutosha kulala upumzike kabla ya safari kuanza.
Kutegemea umri wa watoto, wewe unapaswa kuwa macho muda wote wa safari. Watoto wanayo tabia ya kutaka kusimama na kucheza mkiwa safarini pia hufungua mikanda ya viti vyao ili wapate fursa hii. Iwapo utapitiwa na usingizi, watoto namna hii huhatarisha maisha yao. Iwapo una mtoto zaidi ya mmoja na mkakaa viti tofauti, muombe jirani na mtoto akusaidie uangalizi. Hata hivyo hakikisha kiti alichoketi mtoto kinaonekana kirahisi toka ulipokaa wewe.
Chakula njiani? Unapopanga mizigo ya safari usisahau chupa ya maji ya kunywa na vyakula vinavyobebeka kama mkate, korosho, nk. Tofauti na watu wazima, watoto hula mara nyingi zaidi katika siku na ule utaratibu wa mabasi kuingia migahawani unaweza ukawachelewesha watoto kupata chochote na kuleta kadhia safarini.
Katika kupanga vitu muhimu vya safari tafadhali usisahau nguo za kusitiri baridi hata kama mnasafiri katika msimu wa kiangazi kwani safarini lolote laweza kutokea mkalala njiani. Chukua masweta, ikiwezekana hata shuka na kama mtoto ni mdogo sana beba pia kanga za kutosha. Beba pia tochi kwani unaweza kuihitaji wakati wa usiku. Hakikisha simu yako iwe na chaji ya kutosha pamoja na kihifadhi chaji (power-bank) ikiwezekana. Simu ni kifaa muhimu sana wakati wa dharura. Uwe na safari na mapumziko mema ya mwaka mpya.
Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania.