Malezi mema ndio msingi wa maadili mema

Malezi mema ndio msingi wa maadili mema

Joined
Oct 26, 2024
Posts
5
Reaction score
0
DSC_0195.JPG

Jamii Imetakiwa Kuwa na Mashirikiano Katika Kulea Watoto Ili Kuwakuza Katika Maadili Mema.
Ushauri huo umetolewa na katibu wa kamati za maadili kutoka Jumuiya ya Maimamu Zanzibar JUMAZA Abdallah Mnubi Abass wakati akizungumza na wanawake wa kiislamu huko tomondo mshelishelini Wilaya ya magharibi B Unguja.

Amesema kutokuwepo kwa malezi ya pamoja katika jamii ni sababu moja wapo ya kuporomoka kwa maadili kwa vijana.

Ustadh Abuubakar Ali Mwalimu amesema kutokuwepo kwa usimamizi wa pamoja katika malezi ya watoto kunasababisha kuporomoka kwa maadili katika jamii.

DSC_0191.JPG


Nao baadhi ya wanawake waliohudhuria katika mhadhara huo wamesema kufuata mila na tamaduni za kimagharibi ni sababu moja wapo ya kuoromoka kwa maadili na kutokuwa na ushirikiano katika jamii.

Sambamba na hayo wameitaka jamii kuwalea watoto wao katika malezi ya pamoja ili kukuwa katika maadili mema ya kiislam.
 
Back
Top Bottom