Malezi ya kijana msaada

Malezi ya kijana msaada

Enny

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
962
Reaction score
130
Nina kijana wangu ana soma form one, maendeleo yake ni mazuri sana kwani ameweza kuwa wa 2 kati ya watoto 140. Sasa ili kumpa motisha nilimwambia nitampeleka out siku ya mwisho kabla hajaenda shule na marafiki zake, nilipanga kumpeleka Best Bite au steers kabla hajaenda shule kesho Jumamosi. Lakini kuna tabia moja amefanya imeniudhi sana, msichana wa kazi alikuwa anafanya usafi bahati mbaya katupa kitambaa chake cha kufutia miwani. Ameanza kumtukana huyo msichana, kachukua simu yake na kumwambia hata mpa mpaka amtafutie kitambaa chake.

Sasa nauliza ili kumrekebisha hiyo tabia mbaya, nisimpeleke huko nilikomwaahidi kwaajili ya kumpa motisha au nifanyeje? kwani sipendi awe na tabia hiyo na pia ajifunze uvumilivu kuishi na watu.
 
Mkuu mpeleke huko kwenye ahadi yake, na utumie huo muda mkiwa huko kumwambia kwa upole ubaya wa hasira na kujaribu kutafuta mbinu pamoja ya kuweza kupunguza hasira zake, kama anazo. au kama dhalau basi afundishwe kwa upendo ili ajue binadamu wote ni sawa.
 
Nina kijana wangu ana soma form one, maendeleo yake ni mazuri sana kwani ameweza kuwa wa 2 kati ya watoto 140. Sasa ili kumpa motisha nilimwambia nitampeleka out siku ya mwisho kabla hajaenda shule na marafiki zake, nilipanga kumpeleka Best Bite au steers kabla hajaenda shule kesho Jumamosi. Lakini kuna tabia moja amefanya imeniudhi sana, msichana wa kazi alikuwa anafanya usafi bahati mbaya katupa kitambaa chake cha kufutia miwani. Ameanza kumtukana huyo msichana, kachukua simu yake na kumwambia hata mpa mpaka amtafutie kitambaa chake.

Sasa nauliza ili kumrekebisha hiyo tabia mbaya, nisimpeleke huko nilikomwaahidi kwaajili ya kumpa motisha au nifanyeje? kwani sipendi awe na tabia hiyo na pia ajifunze uvumilivu kuishi na watu.

Am sorry Enny, "...mwana umleavyo...!" hiyo mentality ya 'holding to ransom,' mfano hutamfanyia mtu kitu mpaka afanye jambo ulitakalo, amekuiga wewe.
 
Sit down and talk to your son about his changed behavior.
Mwambie makosa yake,madhara ya makosa hayo,nini anatakiwa kufanya kwenye situation kama hiyo na hatua za kurekebisha pale alipoharibu yaani kumuomba dada msamaha na kuahidi hatorudia tena.
Akifanya hayo bila kusukumwa,mpeleke kule ulikomwahidi coz atakuwa ashajifunza.
 
Mpeleke kama ulivyo ahidi
itasaidia kuwa na muda mzuri wa kumfundisha tabia unayotaka wewe
hata kama amekosea sio kulipiza kisasi ni kutafuta njia ya kumrekebisha
 
Keep promise, mpeleke ulipomuahidi kabla sijakasirika.
 
Am sorry Enny, "...mwana umleavyo...!" hiyo mentality ya 'holding to ransom,' mfano hutamfanyia mtu kitu mpaka afanye jambo ulitakalo, amekuiga wewe.

Yeah it is in the blood vains
 
Am sorry Enny, "...mwana umleavyo...!" hiyo mentality ya 'holding to ransom,' mfano hutamfanyia mtu kitu mpaka afanye jambo ulitakalo, amekuiga wewe.

Ni kweli Mbu,
Kwanini of all the things he could have done to the boy amewaza tu kutomtimizia ahadi yake?
Pengine na mtoto amereact jinsi wazazi wake wanavyoreact kwenye situations kama hiyo yake
 
Ingekuwa ni kipindi
Kile cha msimu ule mama
kasha kushikia malapa halafu anakupa
adhabu baada ya ****** kuwa mekundi..

Nway hakuna cha lelemama
mpe adhabu akifanya na
kumuuomba msaamaha msichana wa kazi
basi mpeleke out.. ama sivyo usimpeleke. Anatakiwa
kujifunza heshima ni kitu cha bure anaweza asome mpaka na
Ma PHD apate lakini kama hana heshima kimekula kwake
 
Mpeleke kama ulivyo ahidi
itasaidia kuwa na muda mzuri wa kumfundisha tabia unayotaka wewe
hata kama amekosea sio kulipiza kisasi ni kutafuta njia ya kumrekebisha

...madhara ya jambo hilo -'Red'-, mtu atakuwa anakufanyia yale uyatakayo ('kuyaona/kuyasikia')
ingawa moyoni huenda wala hana kusudio na hilo.

Kwenye malezi ya watoto tusijisahau kwamba, pamoja na yote 'tutayotakayo' kwao i.e
('pushy parents,') ...nao ni binadamu kamili wenye nia, maoni na matakwa tofauti.

Kama mzazi/wazazi, jukumu letu ni kubalance matakwa na matamanio yao yawe kwenye mfumo sahihi wa maisha kulingana na jamii waliyomo. mfano, hata kama utailea familia yako kwenye mazingira ya kijeshi, si sahihi
kuwaachia wanao wadhani maisha ni 'commands na salutes' pekee.
 
Ina onekana hujazoea kumkaripia au kumkanya kitu chochote, kwa ninavyojua kama anakiwoga au heshima fulani asingefanya hayo mbele yako au kwa msichana wake, nenda nae out umwambie umefurahi sana alivyofaulu ila pia umechukia sana kitend alichofanya na uweke uso wa kumwonyesha umemaanisha ulichosema.Halafu make sure anaenda kanisani au msikitini mara kwa mara apate hofu ya Mungu, Pole sana kulea kazi sana.
 
Nina kijana wangu ana soma form one, maendeleo yake ni mazuri sana kwani ameweza kuwa wa 2 kati ya watoto 140. Sasa ili kumpa motisha nilimwambia nitampeleka out siku ya mwisho kabla hajaenda shule na marafiki zake, nilipanga kumpeleka Best Bite au steers kabla hajaenda shule kesho Jumamosi. Lakini kuna tabia moja amefanya imeniudhi sana, msichana wa kazi alikuwa anafanya usafi bahati mbaya katupa kitambaa chake cha kufutia miwani. Ameanza kumtukana huyo msichana, kachukua simu yake na kumwambia hata mpa mpaka amtafutie kitambaa chake.

Sasa nauliza ili kumrekebisha hiyo tabia mbaya, nisimpeleke huko nilikomwaahidi kwaajili ya kumpa motisha au nifanyeje? kwani sipendi awe na tabia hiyo na pia ajifunze uvumilivu kuishi na watu.

we waozeshe tu ukitaka arekebishike;mpaka anafanya hivyo kuna pazia kubwa nyuma yao mwombe Mungu akupe macho ya Rohoni
 
Dah! Umekosea, palepale wakati anamtukana msichana ungemkanya.
Kwanini unashindwa kumuamrisha amrudishie simu?
Mwambie arudishe, mkanye na mipango mingine iendelee kama kawaida.
 
Jamani Pdidy huyu si mtoto wa Form one halafu unaonekana ulijifunzia kwa HG wewe!! tehetehetehe
 
usipompeleka tu!! utaona atakachokufanyia na wewe, si ajabu akiamka jumapili asikusalimie sijui utamfanyaje.

hawa watoto wa @yahoo.com wana taabu sana!!!

Ila pia vaa Naivera umuulize Bwana kwa maana imeandikwa "Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi"
 
Wewe unamdekeza huyo mwanao nasema kwa uzoefu kwa sababu mie namdekeza sana mwanangu wa kiume kuliko wale wakike na wanajua ha ha ha ha mie napenda watoto wa kiume kweli kuliko wa kike na mtu asiniulize kwanini sababu sitajibu
 
Da Dena msg yangu jana uliipata?
 
Dah! Umekosea, palepale wakati anamtukana msichana ungemkanya.
Kwanini unashindwa kumuamrisha amrudishie simu?
Mwambie arudishe, mkanye na mipango mingine iendelee kama kawaida.
Sorry, mimi sikuwepo nilikuwa kazini na mpaka sasa sijamwona kwani nipo kibaruani, nimepigiwa simu tu.
 
Ina onekana hujazoea kumkaripia au kumkanya kitu chochote, kwa ninavyojua kama anakiwoga au heshima fulani asingefanya hayo mbele yako au kwa msichana wake, nenda nae out umwambie umefurahi sana alivyofaulu ila pia umechukia sana kitend alichofanya na uweke uso wa kumwonyesha umemaanisha ulichosema.Halafu make sure anaenda kanisani au msikitini mara kwa mara apate hofu ya Mungu, Pole sana kulea kazi sana.
Jamani mimi nipo kibaruani sikuwepo hayo yote yaliyotokea, nimepiguwa simu tu toka nyumbani
 
Asanteni sana kwa mchango wenu, michango yenu ni muhimu sana
 
Back
Top Bottom