Malezi ya mtoto introvert

Malezi ya mtoto introvert

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Wakati familia nyingi za nchi zilizoendelea zikijitahidi kuwalea kwa umakini watoto wenye tabia za uintrovert, hali ni tofauti huku Uswahilini. Watoto introvert hukumbana na kadhia ya kulazimishwa kuwa extrovert jambo ambalo haliwezekani.

Lakini kuwa introvert au extrovert si tatizo. Tafiti zinaonesha kuwa asilimia ishirini na tano mpaka arobaini ya watu wote ulimwenguni ni introvert. Asilimia zilizosalia ni extrovert.

Kwa asiyefahamu, introvert ni mtu ambaye kwa asili ni mkimya, mwenye kutafakari kwa kina ambaye mara nyingi hupenda mazingira tulivu hivyo mara nyingi hupenda kukaa peke yake. Hafurahii kukaa muda mrefu kwenye eneo lenye watu wengi na makelele kama sherehe ya harusi. Hata kwa watu wazima ambao ni introvert, mara nyingi wao ndiyo huwa wa kwanza kuondoka kwenye mikusanyiko ya watu wengi kama harusi.

Japo simaanishi kuwa introvert ni bora kuliko extrovert, lakini tafiti zinaonesha kuwa introvert ndiyo wanaoongoza kwa kuwa na "akili" sana. Watu wengi walio kwenye taaluma za kufikirisha sana kama engineering, uhasibu, uandishi wa vitabu, udaktari, n.k., ni introvert.

Ikiwa utagundua mwanao ni introvert, usijisumbue kumtamani awe extrovert . Unachopaswa kufanya ni kumlea kiusahihi katika uintrovert wake. Kwa hiyo:

1. Jenga naye urafiki.
Si wepesi kuwakubali watu kama marafiki zao hata kama ni ndugu zao. Ukiona amekuamini kiasi cha kuwa huru kukujukisha kwa uhuru mambo yake ya siri, ujue ni kwa sababu ameshakuchunguza na kujiridhisha kuwa wewe ni mtu sahihi kukushirikisha mambo yake ya siri. Usiiharibu hiyo fursa.

Ikitokea kwa mfano, kafanya jambo la "aibu" kama kukojoa kitandani, ukifahamu, msaidie ajue kuwa unashirikiana naye kutatua hiyo changamoto bila watu wengine kama wadogo zake kufahamu. Hiyo itamfanya akuamini zaidi na hivyo siku akiwa na tatizo huwa huru kuzungumza nawe.

2. Mpe uhuru wa kuwa kimya. Usimlazimishe kuongea. Mfahamishe kuwa anaweza kukaa kimya kadiri apendavyo, lakini akiwa amekasirishwa au kuchukizwa asikae kimya.

3. Jitahidi kumpa majibu ya kumridhisha anapokuuliza maswali.
Introvert hawapendi majibu mepesi. Ukiona anapenda kukuuliza maswali, ujue umekuwa ukimpa majibu yaliyoshiba. Lakini akiona majibu yako ni mepesi, hatakuambia bali atakuonesha kwa vitendo. Ataacha kukuuliza.

Ni kawaida kwa watoto introvert kupenda kuwa karibu na watu wanaowaamini wamewazidi uelewa ili waweze kuwauliza maswali. Kama mzazi hatakidhi haja yake, hatahangaika kuwatafuta mbali watu wa aina hiyo.

4. Uulishe ufahamu wake kwa "picha" nzuri. Kwa kuwa ni watu wa kufikiria sana, ni muhimu wawe na taarifa nzuri ya kuwatafakarisha. Msomee vitabu mbalimbali vizuri na kumwonesha video za taaluma mbalimbali. Hiyo itakusaidia kubaini vitu anavyovipendelea maishani mwake. Ukiona, kwa mfano, anavutiwa sana na masuala ya kiteknolojia, usisite kumtafutia vitu vya kuchezea vinavyoendana na teknolojia. Akishajua kusoma, mtafutie vitabu vinavyoendana na mambo anayoyapenda.

5. Mtie moyo katika maeneo anayoonekana kufanya vizuri.
Namna nzuri ya kumtia moyo aendelee kuimarika katika mambo mema ni kwa kumsifia, na hata wakati mwingine kumpa zawadi pale anapofanya vizuri. Ukiona anapenda sana kusoma vitabu mpongeze. Akiwa na tabia ya muchokonoa vifaa vya kielectronocs usimkemee, badala yake umwandalie mazingira salama na wezeshi ya kufanya hayo. Huwezi jua, anaweza akaibuka mgunduzi angali mtoto mdogo.

Nihitimishe kwa kukumbusha kuwa introvert si ugonjwa, na wala si watu wenye aibu. Aibu anaweza kuwa nayo mtu yeyote bila kujali kama ni introvert au extrovert. Ukiwa una mtoto introvert, chukulia kama ni mmoja wa watoto wenye bahati na umlee kiusahihi aweze kuifikia hatma yake njema.
 
zamani wengi wao walikuwa wanakufa masikini licha yakuwa walikuwa wagunduzi wakubwa!,kuna watu kama Tesla wangekuwepo karne hii wangekula mema ya kazi zao mpk wafaidi!
walau sasahivi wananufaika usimamizi mzuri,ni moja kati ya watu muhimu sana wakitumika vyema.
 
zamani wengi wao walikuwa wanakufa masikini licha yakuwa walikuwa wagunduzi wakubwa!,kuna watu kama Tesla wangekuwepo karne hii wangekula mema ya kazi zao mpk wafaidi!
walau sasahivi wananufaika usimamizi mzuri,ni moja kati ya watu muhimu sana wakitumika vyema.
Tunawasiadiaje wa hapa kwetu ili tuufaidi uwezo wao na wao wafaidi matunda ya fikra zao?
 
ni ukweli mtupu mimi nilipokuwa mdogo nilikuwa nikikaa peke yangu naweza kutungu movie kichwani mwanzo mpka mwisho na kama inahuzunisha machozi yatanitoka kabisa
Unakitumiaje kwa sasa hicho kipaji?
 
Hii hali inanitesa sana.. ni upumbafu mtupu ni ukilema, nateseka sana na huu upumbufu..

Nimetoka job kuna kipori napenda sana kukaa mida ya jioni siwez kabisa kuwa na marafiki, ni mateso tu
 
Back
Top Bottom