Malezi ya wazazi wa siku hizi na dosari zake!

Well said
 
Wanawake wenzio wameiona hii. ..I bet watanuna
 
Hahaha haaa hahaa. .Aibu kubwa sana hii kwa wazazi wanao jitambua
 
Hii ndio sababu moja wapo iliyo changia 'Jamii kuwa na watu kama kina amber rutty. Mariam birian. Juma okelo. Na vijana wengine wanaoshinda mitandaoni na kutukana watu matusi mazito mazito na kashfa juu Wema sepetu akiwa ni moja ya product ya malezi ya aina hiyo "

Jamii inapokuwa na majority kubwa ya watu wenye Tabia hizo. ..Taifa linaingia kwenye dosari kubwa na hatimae Lita onekana kuwa ni Taifa la watu wa hovyo ..wasiojua mantiki ya ustaarabu
 
Maranyingi watu hukumbuka pale walipolelewa vizuri kwa kufundishwa adabu , heshima na ubinadamu kuliko kule walipodekezwa na kuharibiwa tabia

Wanakumbuka hata ikiwa ni kwa shangazi, mama mdogo, bibi au ndugu japo wakati huo wakiwa wanafunzwa adabu walikua wanadhani wanaonewa au wanateswa
 
Ni kweli kabisa usemayo mkuu
 
Wewe acha tu mkuu ' tanzania ni Jahazi lililo Toboka. .kama halitofanyiwa service basi tusishangae tutakapoona linazama
Bahati mbaya sana wanaopigania maadili kwa watoto wanaonekana wamepitwa na wakati kwa hiyo kama ni jahazi la maadili limeachwa tu lifuate upepo utapolipeleka

Miaka kadhaa ijayo zitakuja sheria kama za nchi za magharibi, kwamba mtoto akiadhibiwa na mzazi anaenda kushtaki ustawi wa jamii na mzazi anaadhibiwa😃
 
Daaah! Inasikitisha sana na yote hayo vyanzo ni sisi wazazi wa kidigitali kwani tunawalea watoto kimadekezo kuliko kawaida.

Na ndio sababu mtoto anaweza mkosea mzazi akachapwa na ikitokea mtoto kakasirika basi mzazi atakwenda kumbembeleza yaishe wakati zamani hayakuwepo haya.
 
Hivi Shadeeya ushawahi kumuomba radhi mwanao kisa kanuna baada ya kumuadhibu? Au wewe mtoto kwako hakanywi?
 
Wazazi wa kiume wanakuwa wapi katika malezi?
mtoto anapokuwa mdogo ni wa mama, kwa maana ya kwamba 80% ya malezi yake ya udogoni yanabebwa na mama. Na ndio maana hata sheria inatuambia kwa wazazi wanaoishi mbali mbali baba anaruhisiwa kuishi na mtoto akiwa tayari ana umri wa 6+.

Hivyo mtoto yeyote akiwa na mitabia ya ajabu obvious lawama nyingi zinaenda kwa mama kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake vizuri.
 
wazazi wa siku hizi priority kwao ni kuona mtoto anakua huku akiongea kingereza kwa ufasaha, suala la nidhamu kwao sio issue kabisa.

Kwenye hizi day care centers matoto mengi yana vichwa vigumu kweli hayasikii ukiyakataza kitu, halafu yakiguswa tu na kiboko kesho yake mama mtu huyu hapa anakuja kulalamika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…