Malezi ya wazazi wa siku hizi na dosari zake!

Malezi ya wazazi wa siku hizi na dosari zake!

Daaah! Inasikitisha sana na yote hayo vyanzo ni sisi wazazi wa kidigitali kwani tunawalea watoto kimadekezo kuliko kawaida.

Na ndio sababu mtoto anaweza mkosea mzazi akachapwa na ikitokea mtoto kakasirika basi mzazi atakwenda kumbembeleza yaishe wakati zamani hayakuwepo haya.
Wazazi wetu hawakuwa na madigriii wala ma-phd lakini walikuwa ni walezi wazuri sana, pamoja na wao kutokuwa na ufahamu mkubwa wa mambo mbali mbali yanaihusu dunia hii lakini waliweza kulea watoto wao katika misingi thabiti ya kinidhamu na uwajibikaji ambayo imewajenga Leo hii tunaona matunda yake.

Sasa wazazi wa siku hizi ambao wengi wao wamebahatika kupata elimu na ufahamu mkubwa wa mambo mbali mbali, wazazi ambao pengine ndio wangeweza kutuletea kizazi bora kupitia malezi bora sababu ya elimu kubwa waliyonayo. Badala yake wao ndio wamekuwa wazazi wenye malezi ya ovyoo kupindukia.

Wengi wao wamekuwa wakiwalea watoto kwa kufuata kile wanachokiona kwenye TV shows hasa za kigeni, na sio kufuata waledi na tamaduni sahihi. Kuna siku nilikuwa kwenye saloon moja hivi hapa mjini akaja dada mmoja hivi ameongozana na mwanae kwa makadirio ni kama kana 5 yrs hivi pamoja na mume wake, ilipofika zamu yao kakanyoa kwanza katoto kao, kalivyomaliza kunyoa akafuata baba mtu.. wakati baba mtu ananyoa kale katoto muda wote kalikuwa kanazunguka tu mle ndani huku kakishika chochote alichoweza kukifikia... muda wote huo mama mtu alikuwa anafanya kazi ya kukataza tu "Edson plzz stop it,...edson plzz i will beat u..edson" wakati huo mama mkononi kashika simu yake yuko insta na amekaa, baba mtu yuko kimya tu. Kwa baadae sana ndio nikaona baba mtu anatoa simu yake akakakabidhi kakaanza kuangalia katuni kupitia youtube. Kale katoto kaliacha gumzo sana walivyoondoka.
 
Meeyah is right sie yametukumba kwa kuwa mbali na mabinti zetu
Huyo anayebisha sidhani hata Kama anaye mtoto. Nimejionea mengi. Uwepo wa baba ni muhimu kwa watoto wote. Mtoto wa kiume hata kama baba hayupo basi awepo mwanaume kwenye hiyo nyumba. Ila mtoto wa kike anahitaji baba
 
Duu! mleta uzi umenigusa.
Kwanza niseme uwazi mimi ni muumini wa kanisa katoliki. tuna utaratibu wa kusali jumuiya. kwa maana ya kusali nyumba kwa nyumba za wakatoliki kulingana na utaratibu wa kanisa.
Kuna siku tulienda kusali kwa dada mmoja ni Dr. wa hospitali ya BMC, uwiiiiii jamani wale watoto walinikera!!
Yaani sala zinaendelea mara wanakwenda pale mbele kwenye "altare" wanaanza kuvuta vitambaa, mishumaa, bibilia n.k" mara vinaanza kuimba nyimbo za shuleni, mara vinatuambia tunyanyuke kwenye viti vya nyumbani kwao, mama yao sasa ambaye ni Dr. yuko tu "yuuu, yuuuu plisi, plisi...)
Nimeapa siku nyingine wakipanga kusali jumuiya kwa Dr. siendi maana nitawafinya wale watoto wake
😡😡😡😡😡😡😡
Kwenye jumuiya[emoji3][emoji3][emoji3] kuna siku nilinusurika kumwagiwa mchanga na mtoto ..umenikumbusha mbali aisee yule mtoto alikua anaharibu kila kitu , sisi kipindi tuko wadogo aje tu mgeni uchelewe kumuamkia au umuamkie afu ukosee baba mdogo umwite mjomba unaambiwa kajikatie fimbo.. mkong'oto utakaoupata hutasahau tena
 
Huyo anayebisha sidhani hata Kama anaye mtoto. Nimejionea mengi. Uwepo wa baba ni muhimu kwa watoto wote. Mtoto wa kiume hata kama baba hayupo basi awepo mwanaume kwenye hiyo nyumba. Ila mtoto wa kike anahitaji baba
kwamba uwepo wa baba kwa mtoto mdogo ambae ndio anaanza kukua ni muhimu kuliko hata uwepo wa mama..!! nashawishika kuamini haya maneno yanatoka kwa mwanamke mvivua anayejua kuzaa tu na sio kulea.
 
Ila huu uzi umenikumbusha katoto ka Dada angu ..kale katoto kamelelewa ovyo kabisa..lilitokea tukio kama ilo la msiba tuko msibani katoto kanamwambia mama ake waondoke..mama ake anakaambia subiri tuzike tutaondoka mtoto acha acharuke anamvuta mama ake nguo yani ili mradi amkere wanyanyuke waondoke..yule dada baada ya kuona kero zimezidi akampiga kale katoto kofi .

Kakaanza kujiliza kanabembelezwa kanazidisha sauti mama ake akawa kama anamnon'goneza katoto si kakaropoka "toka hapa ndio maana baba anakupigaga"

Aibu niliona mimi
 
Kuna mtoto jirani hapa, ananiogopa na kunipenda kuliko baba na mama yake.
Hawezi kujilizaliza mbele yangu kama afanyavyo kama baba na mama yake.
Nilichogundua moja ya sababu ya malezi mabaya kwa hawa watoto wetu ni malazi mabaya ya sisi wazazi wao kutoka kwa walezi wetu, chunguzeni hili.
 
Huyo anayebisha sidhani hata Kama anaye mtoto. Nimejionea mengi. Uwepo wa baba ni muhimu kwa watoto wote. Mtoto wa kiume hata kama baba hayupo basi awepo mwanaume kwenye hiyo nyumba. Ila mtoto wa kike anahitaji baba
Wewe mama una uzoefu! Achana na mitoto inayobalehe hapaJF. Huwezi amini sasa najuta kukuza binti bara tofauti. Ila hakuna kulala mwanaume lazima upambane ili ubadili upepo
 
kwamba uwepo wa baba kwa mtoto mdogo ambae ndio anaanza kukua ni muhimu kuliko hata uwepo wa mama..!! nashawishika kuamini haya maneno yanatoka kwa mwanamke mvivua anayejua kuzaa tu na sio kulea.
Umeshazaa mtoto akafika umri wa zaidi ya 25?
 
Ila huu uzi umenikumbusha katoto ka Dada angu ..kale katoto kamelelewa ovyo kabisa..lilitokea tukio kama ilo la msiba tuko msibani katoto kanamwambia mama ake waondoke..mama ake anakaambia subiri tuzike tutaondoka mtoto acha acharuke anamvuta mama ake nguo yani ili mradi amkere wanyanyuke waondoke..yule dada baada ya kuona kero zimezidi akampiga kale katoto kofi .

Kakaanza kujiliza kanabembelezwa kanazidisha sauti mama ake akawa kama anamnon'goneza katoto si kakaropoka "toka hapa ndio maana baba anakupigaga"

Aibu niliona mimi
Unajua ni nini hapo? Hayo ni matunda ya mpasuko kati ya mama na baba. Kama sikosei katoto hako ni kasichana
 
Back
Top Bottom