Boss ni mzazi mwenyewe tu sisi tumelelewa na mzee pamoja na maza tena home mzee Alikuwa hajui kupiga wala kugombeza mtoto na haongeagi tu.... Ila maza alitunyoosha kweli kweli tena mnoo akikutuma umekataa stiki, umesusa kula fimbo, ukiomba kitu kwa mtu akijua tu kipigo, umetumwa sehemu umechelewa kurudi fimbo,yaani kama vitani vile dingi hana huo Muda maza anakalisha watoto wa kiume jikoni mzee anawaka kwa nini!, maza anamwambia mimi ndiye niliyezaa we subiri tu nifundishe watoto, aseee yaani maza katuburuza kweli kweli hakuna mtoto mtukutu kati yetu.... Yaani ni adabu mwanzo mwisho.... Mimi nasema mama ndiye zaidi kwenye malezi sababu nimeyaona sijahadithiwa...