Malezi ya wazazi wangu yameniathiri vibaya sana

kaisar19

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2021
Posts
274
Reaction score
488
Nimelelewa kwenye mazingira ambayo sikupewa nafasi ya kuchanganyika na watoto wenzangu. Baada ya kuoga na kupaka mafuta ilikuwa ni kukaa ndani hadi muda wa kula usiku. Sikuwahi kuwa na marafiki wa kucheza nao, kupiga stori au kufanya mambo ya kawaida ya utotoni.

Baada ya kuanza maisha kujitegemea, naiona athari yake. Sina ujasiri wa kuanzisha mazungumzo na watu au kujichanganya nao kirahisi.

Wengi hunitafsiri vibaya, wakidhani nina majivuno au dharau, kumbe ukweli ni kwamba ninapata hofu na kukosa ujasiri ninapokuwa mbele za watu.

Nakumbuka siku moja nilipotea maeneo ya Kariakoo. Badala ya kumuuliza mtu njia, nilizurura kwa masaa mengi kwa sababu tu sikuwa na ujasiri wa kuomba msaada. Jioni ilinikuta bado natafuta njia, hadi nikajikuta nimetokea maeneo ya Posta baada ya kupita kwenye maghorofa mengi.

Je, kuna watu wengine waliokulia kwenye malezi ya aina hii na sasa wanapitia changamoto kama hizi? Mmewezaje kujenga kujiamini na kujifunza kuchangamana na watu?
 
Hahahaha Mkuu hata kama ndio ushindwe kuuliza? Vipi kama haja umekubana inamaana utajipupulia kisa unaogopa kuuliza huduma ya choo ilipo
 
Inashangaza sana kuona mtu mzima unasingizia malezi ya miika 15 iliyopita wakati sasa hivi una akili yako timamu ya kujiongeza.
HIvi wewe unajua PTSD kweli?

Msiwe mnapenda kuongea faul words kwa watu. Inawaongezea maumivu na anxiety
 
Mkuu, kama utataka mtu wa kukusaidia njoo pm...

Ila inapaswa utambue malezi yamekuharibu kwa namna ambayo hata wewe mwenyewe huwezi kuona... Tayari mwili umesha adapt uhalisia ulio kulia... So ili ubadilike lazima ufute huo uhalisia...

Na haita chukua siku wa miezi...

Inaweza kuchukua miaka kadhaa.

Na hii ni endapo Utakubali Kuanza safari ya mabadiliko..

Kama una uwezo nyumbani tafuta therapist..

Au ingia YouTube na uanze kuangalia video za CBT(cognitive behavior therapy)

Nakutakia uponyaji na maisha yaliyo bora na yako mbeleni.
 
Back
Top Bottom