Mali aliyoikuta mwanamke inaweza kugawanywa sawa endapo mmeachana?

Mali aliyoikuta mwanamke inaweza kugawanywa sawa endapo mmeachana?

jewenkela

Member
Joined
May 25, 2020
Posts
92
Reaction score
169
Ndugu wapendwa,

Niligombana na mke wangu, kwa shinikizo la wazazi wake akanipeleka polisi na kufungua kesi ya jinai kuwa nimempiga so nikawekwa mahabusu na kutoka kwa dhamana.

Baada ya ushauri alihiari kufuta kesi lakini baba yake akadai nimrudishie gharama aliyoitumia kuja kutatua matatizo ya binti yake.maana alopokuja hakutaka kufikia kwangu ila alifikia guest. Nilikataa baadae akaomba kesi iendea mahakamani aendelee na jinai ya bintie.

Mahakamani tulishauliwa na wazee wa mahakama wife akafuta kesi lakini baba yake akaendelea kudai nimlipe gharama za usumbufu kwa ushauri wa wazee wa baraza ikabidi nimlipe pale pale ili mambo yaishe.

Sasa nimekaa na kutafakari kuwa huyu mwanamke hanifai japo tuna mtoto mmoja. Nafikiria kumpa taraka. Sasa shida inakuja kwa kuwa wazazibwake wamenionyesha kuwa ni wenye tamaa lazima watamshauri tugawane mali. Na hii mali kiwanja na nyumba alivikuta nimeandikisha majina yangu.

Sasa je, kuna uwezekano wa kugawana mali aliyoikuta?
 
Kwa watu wa kusini bwana (mwela ndonde na makonde) pasu kwa pasu ndio sheria yao, no matter what no matter how

Mpaka imekuwa kama fashion sasa mabinti wakiolewa wanangoja mambo yakianza kuwa kwenye mstari (ufuta, viwanja nyumba/mashamba na assets) tayari hakutaki anataka talaka
 
Mkuu huyu ulioa au uliokota baa?

Je, ni kweli ulimpiga?(hata kama ni kofi 1)

Mwambie achukue kila anachoona kinamfaa ili uwe na amani.
Ila hapo zitahesabiwa mali mlizochuma wote.
 
Sina hakika lakini nafikiri hana haki navyo kwani hamkuchuma wote, pili kwa nguvu zao za jinsia anaweza kukupotezea muda za kwenda mahakamani hivyo kukata mzizi wa fitina kwa usiri bila kumweeleza uza nyumba na kiwanja halafu kimya kimya nunua kiwanja kingine kwa jina la nduguyo na jenga huko
 
Kwa watu wa kusini bwana (mwela ndonde na makonde) pasu kwa pasu ndio sheria yao, no matter what no matter how

Mpaka imekuwa kama fashion sasa mabinti wakiolewa wanangoja mambo yakianza kuwa kwenye mstari (ufuta, viwanja nyumba/mashamba na assets) tayari hakutaki anataka talaka
Mkuu umewasahau wangindo,nimeishi nao sana hapo liwale wanatabia hii pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa watu wa kusini bwana (mwela ndonde na makonde) pasu kwa pasu ndio sheria yao, no matter what no matter how

Mpaka imekuwa kama fashion sasa mabinti wakiolewa wanangoja mambo yakianza kuwa kwenye mstari (ufuta, viwanja nyumba/mashamba na assets) tayari hakutaki anataka talaka
Kwani kuna sheria ya watu wa kusini na watu wa srhemu nyingine za Tanzania..!? Nijuacho, mali inayogawanywa ni ile iliyopatikana wakati mkiwa pamoja, iliyopatikana kabla ya kuwa mke na mume haihusiki kwenye kugawanywa... UNLESS MHUSIKA AAMUE
 
Sina hakika lakini nafikiri hana haki navyo kwani hamkuchuma wote, pili kwa nguvu zao za jinsia anaweza kukupotezea muda za kwenda mahakamani hivyo kukata mzizi wa fitina kwa usiri bila kumweeleza uza nyumba na kiwanja halafu kimya kimya nunua kiwanja kingine kwa jina la nduguyo na jenga huko
Ni kweli, kama mtu hana muda wa kuhudhuria mahakamani, anaamua tu PASU KWA PASU halafu anasepa... Maana unaweza kuta mtu anapoteza zaidi ya nusu anayohofia kuigawa kwa kuitumia muda mwingi kwenye kesi
 
Mkuu Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ina kifungu kinachosema wazi kabisa kua "Mali ulizochuma kabla hujamuoa ni zako, lakini mlizochuma wakati mko kwenye ndoa hizo ni zenu wote....So ukifuata sheria hana chake ila ukitumia busara waweza muachia chochote kitu kwa kua ni mama mtoto wako.
 
Mkuu huyu ulioa au uliokota baa?

Je ni kweli ulimpiga?(hata kama ni kofi 1)

Mwambie achukue kila anachoona kinamfaa ili uwe na amani.
Ila hapo zitahesabiwa mali mlizochuma wote.
Nilioa mkuu tena na mahali yote ililipwa bila chenga. Kumpiga ni kweli nilimpiga japo ilokuwa hasira na kwa nia ya kurekebishana
 
Endapo mali hizo mmechuma kwa pamoja basi sheria itakutaka kufanya hiyo
 
Sina hakika lakini nafikiri hana haki navyo kwani hamkuchuma wote, pili kwa nguvu zao za jinsia anaweza kukupotezea muda za kwenda mahakamani hivyo kukata mzizi wa fitina kwa usiri bila kumweeleza uza nyumba na kiwanja halafu kimya kimya nunua kiwanja kingine kwa jina la nduguyo na jenga huko
Hapa atakuwa ametengeneza kesi nyingine......maana nyumba wanayoishi inahesabika kama ya familia. Na mteja kama anajua una mke hatakubali kununua bila kuhakikisha mke karidhia
 
Tumia hekima zako tu mkuu mmpe japo robo ya hizo Mali kwakuwa ni mama mtoto wako, usimuache mtupu si busara

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Kwa namna wazazi wa mke wangu hasa baba yake walivyo nitenda sina hata chembe ya huruma kwake. Kama sheria hairuhusu yy kutopata mgao wowote basi hapati chochote kutoka kwangu. Kiukweli namchukia mke wangu lakini zaidi nawachukia sana sana wakwe zangu. Atabaki tu kupata labda hiyo pesa ya matunzo ya mtoto mpaka mwanangu atakapofikisha umri wa kukaa na mm
 
Iko hivi. Hilo la kugawana Nusu kwa Nusu ni kama wamelipotezea ili kuondoa Ndoa kuuvunjwa kisa mali.

Mwanamke atatakiwa athibitishe mchango wake na ushahidi.

Kuhusu kupika Hela wewe ndiye watoa.
Kuhusu kulea hata usingekuwepo bado angelea.

Kinachofanyika Kama mtoto yupo basi utatakiwa uwe watoa matunzo kutokana na uwezo wako kifedha.

Haya ni kutoka Ustawi Wa Jamii
 
Timua tu hiyo pimbi.. wanawake wa sikuhizi vichomi Sana na dawa yao ni kuwaacha wakakutane na vichomi wenzao.. yaan haiingii akilini Mwanaume unakua mpole na mpenda Amani Ila jianamke ndo kila siku linatafuta magomvi..!?

Hata wakichukua Mali zote.. ukipambana unazirudisha Tena hata zaidi ya Hizo.. tanguliza Aman ya Roho mkuu
 
Tengeneza mazingira akufumanie hata na changu tu,atapata hasira ataondoka,akiondoka,umemkula kwake!
Njia nyepesi tu Wala usihangaike.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom