Ila inaonekana wee huna adabu na mbabe na hujui maana ya mke na ndoa.
Kwa mila zetu tumezoea mume kumfata mke kwao hata Kama katoroka, utawekwa kitimoto kama mke wa kurudi basi atarudi kama si wa kurudi hupewi.
Kwa jinsi ulivyo....mpe tu talaka....hakika kapata mume kichomi.
Kama kweli Mali alizikuta basi ni zako , ila atapata asilimia ndogo hata 10 hivi, hatotoka bure.
Yaani ww kwa komenti zako hizi unazidi kunitia hasira na kichefuchefu. Et kwa mila zetu, unajua maana ya mila ww au umekurupuka tu kwa kuwa ni mwanamke mwenzio. Nina mashaka pia na unavyoishi na mmeo kama umeolewa.
Ukiongelea mila ni wapi mila zetu zinasema mke akigombana na mmewe breki iwe kwao badala ya kukimbilia kwa wakwe zake? Inatakiwa uende kwa wazazi wangu ikishindikana ndo uende kwenu.
Sasa unagombana na mwanaume alafu unakimbilia kwenu wazazi wako wanakupokea unawajaza uzwazwa bila kujua chanzo cha ugomvi wanakupeleka polisi ukamfungulie mmeo kesi ya jinai hata bila mmeo kujua wala kuitwa kwenu angalau kuyasuruhisha.
Mmeo anawekwa mahabusu, mnafikishana mpaka mahakamani lakini mbaya zaidi baba yako anamdai mmeo gharama za kuja kusuruhisha ugomvi tena kwa lazima utafikiri mmeo ndo amemuita tena kwa vitisho kuwa usipomlipa hafuti kesi, pumbavu kabisa!!!!
Baba mkwe unaondoka bila kufika kwangu wakati ni maeneo hayo hayo tu ulifikia tena gest kuendelea na shauri la binti yako ili umfunge mkweo, kweli!!!!?
Leo hii eti nitangulize tumbo langu kumfuata mwanamke ambae kwa kushirikiana na wazazi wake amenidharirisha vya kutosha!! hicho kitu hakipo, labda aje awaombe msamaha ndugu zangu, wazee wa mahakama alikoenda kunidharirisha alafu aje amalizie na mm ndo naweza kumfikiria lakini sio kumsamehe moja kwa moja.
Na hata mm nikienda kumuona mwanagu sifikii kwake. Ntafikia kwa mjumbe ambako ataitwa aje nimuone mwanangu then achukue mahitaji ya mtoto baadae kila mtu hamsini zake.
Mapenzi ni kubembelezana lakini huwezi kubembeleza kisicho bembelezeka.