Mkuu wa utawala wa ijeshi nchini Mali Assimi Goïta siku ya Alhamisi ameidhinisha sheria inayompa mamlaka ya miaka mitano ya urais, ambayo yanaweza kufanyiwa upya "mara nyingi inavyohitajika" na bila uchaguzi.
Mkuu wa serikali ya Mali amejipa mamlaka ya miaka mitano ya urais, ambayo yanaweza kufanywa upya "mara nyingi iwezekanavyo" na bila uchaguzi, katika sheria iliyowekwa wazi siku ya Alhamisi.
Uidhinishaji wa Jenerali Assimi Goïta wa hatua hiyo ulitarajiwa na wengi kwa siku kadhaa, na unakuja baada ya bune iliyoteuliwa na jeshi la nchi hiyo kupitisha mswada huo wiki iliyopita.
Sheria hiyo, ambayo ilifichuliwa kwa umma baada ya kutiwa saini na Goita siku ya Jumanne, inamruhusu kuongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi hadi angalau mwaka 2030, licha ya ahadi ya awali ya serikali ya kijeshi kurejea utawala wa kiraia mwezi Machi 2024.
Ni moja ya mfululizo wa vizuizi vya uhuru vya uongozi wa kijeshi wa Mali kuimarisha mamlaka yake katika taifa la Saheli lililoathiriwa na wanajihadi.
Baraza la Mawaziri lilikuwa tayari limepitisha hatua hii mwezi uliopita.
Chini ya sheria hii, Goita ataweza kuhudumu kama mkuu wa nchi kwa muhula wa miaka mitano, unaoweza kurejeshwa mara nyingi iwezekanavyo, hadi nchi itakapokuwa na amani.
Goïta alipochukua mamlaka, alisisitiza kujitolea kwa Mali katika kupambana na ghasia za wanajihadi na awali aliahidi kurejea kwa utawala wa kiraia.
Goïta alisherehekewa katika baadhi ya maeneo kama shujaa ambaye angeweza kuleta wokovu katika nchi yake ya Afrika Magharibi yenye matatizo.
Lakini hatimaye alishindwa kutimiza ahadi yake ya kuachia madaraka kwa raia waliochaguliwa, jambo ambalo lilipaswa kufanyika mwezi Machi 2024.
Mapema mwaka huu, mashauriano ya kitaifa yaliyoongozwa na utawala wa kijeshi yalipendekeza kutangazwa Goïta kama raia bila kura kwa muhula wa miaka mitano unaoweza kurejelewa upya.
Mkutano huohuo—uliosusiwa na makundi mengi ya kisiasa—pia ulipendekeza kufutwa kwa vyama vya siasa na kubanwa kwa kanuni za kuundwa kwao.
Baadaye, utawala wa kijesi ulitangaza mnamo Mei kufutwa kwa vyama na mashirika yote ya kisiasa, na pia kupiga marufuku makusanyiko.
Kuendelea kubanwa kwa nafasi za kiraia nchini Mali kunakuja huku mamlaka ikisisitiza kwamba nchi hiyo iungane nyuma ya jeshi.
Utawala wa Goïta uliashiria mabadiliko katika uhusiano wa Mali na nchi za Magharibi. Nchi hiyo imekata uhusiano na Ufaransa na washirika wengine wa zamani na kugeukia Urusi.
Mali na majirani zake wanaoongozwa na Burkina Faso na Niger wameungana kuunda shirikisho lao, Muungano wa Nchi za Sahel (AES), na wametangaza kuunda kikosi cha pamoja cha wanajeshi 5,000 kwa ajili ya operesheni za pamoja za kijeshi.
Wakati huo huo washirika wake mamluki wa Urusi kutoka kikosi cha Africa Corps, waliopewa jukumu haswa la kuwasaka wanajihadi, mara kwa mara wanashutumiwa kwa ukiukaji wa haki dhidi ya raia pamoja na jeshi la Mali.
Tangu mwaka wa 2012, Mali imekumbwa na ghasia zinazofanywa na makundi ya wanajihadi yenye mafungamano na al Qaeda na kundi la Islamic State, pamoja na mashirika mengine ya uhalifu.
Mashambulizi yameongezeka katika wiki za hivi karibuni.
Licha ya ghasia nyingi nchini Mali, Goïta anasalia kuwa maarufu kwa sehemu ya watu, ambayo inamwona kama mbunifu wa mageuzi na uhuru mpya.