Mali Vs Tanzania | 2025 Women’s Africa Cup of Nations | Group C | 07.07.2025

Meja Jenerali Isamuhyo

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
3,709
Reaction score
10,896
Wakuu hamjambo,

Usiku wa leo Saa 4:00 kwa masaa ya Afrika Mashariki, Timu yetu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) itashuka dimbani dhidi ya Mali katika mchezo wa AFCON ya Wanawake huko nchini Morocco.

Huo utakuwa mchezo wetu wa kwanza katika kundi C ambalo pia kuna timu za South Africa pamoja na Ghana.

Tuitakie heri nyingi timu yetu ya Taifa, updates zitakuwepo hapa jukwaani.

Mchezo utakuwa mubashara DStv na Azam Sports 1HD.
 
Ni kukaza tuwapige Hawa na waghana msouth sio rahisi ku battle nae ili tuvuke
 
Mbona kwenye squad list sijamuona Clara Luvanga!? Kuna changamoto yoyote?!inawezekanaje moja kati ya top strickers walio na magoli mengi msimu huu kwenye ligi ya Saudi Arabia akakosekana?!

Aisha Masaka najua ni injury (anachezea Brighton and Hove Albion)

Opa Clement najua alipata yellow kadi kwenye mechi za kufuzu..Tumekosa watu wa maana sana katika mchezo wa leo
 
Namuona jukwaani
 
Dah! Sijui niwatakie tu ushindi! Sijui nipotezee! Maana hawachelewi kuwa kama wale kaka zao kichwa cha mwendawazimu.
 
#TikiKwaSamia

Kufungua milango ya uwekezaji kwa sekta binafsi kulikofanywa na Serikali kuwaleta na kuvutia zaidi wawekezaji binafsi katika sekta ya bandari kumeleta na inatarajiwa kuleta zaidi matokeo chanya nchini, pamoja na watumiaji wa bandari za Tanzania.
 
Mkuu hujui kwanini hachezi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…