Sahihi kabisa haswa CHADEMAHii itafanyika wapinzani wakichukua nchi la sivyo ni ngumu
Ile ripoti haitakuja kusomwa KAMWE. Mwendazake alikuja moto sana kutaka kuiweka hadharani, lakini akakuta waliokuwa wamehodhi zile mali za chama ni watu wanene sana ndani ya CCM (na wengine ndo walimfikisha pale alipokuwa), akaishia kuufyata pamoja na ukali wake wote! Kumbuka kwamba chama KINA WENYEWE.Kwani ripoti ya uhakiki was Mali za chama itasomwa lini?
Bashiru alikuwa Mkiti wa uhakiki,sasa inakuwaje chama kongwe taarifa hatupati.
Viwanja vyote vya michezo nchini wamejitwalia kiharamu. Unatakiwa ifike mahali hizi mali zitaifishwe.Ni mali nyingi sana Chama hiki kimejimilikisha kama tunavyoona kila CCM anaepata uongozi serikalini nae hukwapua mali na hata kugonga milango ya BOT na kufanya mazabe mpaka hufanikiwa kumega ,tumesikia kutoka kwa mkaguzi ya kuwa kuna hela haioni...
Kweli aiseee,yaani kama vile viwanja kuna pesa watz wote tulilazimika kuchangia kupitia bei za bidhaa mbalimbali zilizokuwa tunanunua kama sabuni,mafuta,sukari ili vijengwe.... ilibidi tuwe wapole tu ....Viwanja vyote vya michezo nchini wamejitwalia kiharamu. Unatakiwa ifike mahali hizi mali zitaifishwe.
Inashindikana nini kutaifisha mali walizochuma watanzania pamoja, wakati ilikuwa rahisi kutaifisha shule za mashirika ya dini, au mkoloni mweusi anatisha kuliko mkoloni mweupe?
Ndio maana Chadema hawajengi ofisi. Wanaogopa hoja kama hizi.Ni mali nyingi sana Chama hiki kimejimilikisha kama tunavyoona kila CCM anaepata uongozi serikalini nae hukwapua mali na hata kugonga milango ya BoT na kufanya mazabe mpaka hufanikiwa kumega, tumesikia kutoka kwa mkaguzi ya kuwa kuna hela haioni.
Na ndio tukaona hakuna MCCM anaeendelea, mwisho wao wengi huumbuka na kuadhirika mchana kweupe, tunawaona wanavyoshikana mashati na kukwidana eti wanapelekana mahakamani, nchi hii ina maajabu sana, naukumbuka msemo usemao mwenye nguvu mpishe.
Aibu kila uongozi unaoingia unasonyesha dalili za uongozi uliopita walikuwa na vibaka wakabaji wauawaji.
CHADEMA wanajenga ofisi kwa nguvu za wanachama wao hivyo zitabaki kuwa za chama tofauti na CCM baadhi ya nyumba zao na viwanja vyote vya mpira na sabasaba vimejengwa kwa fedha za umma na rasilimali za serikali kama watumishi na vyombo vya ujenzi na pia wananchi wa kawaida na pia wafanyabiashara ambao wala si wanachama wao!Ndio maana Chadema hawajengi ofisi. Wanaogopa hoja kama hizi.
Utasikia jina la uwanja wanatanguliza ccm, ujue tayari wameuchukua huo, Wa hivi karibuni ni ule wa Jamhuri Dodoma, Walianza kuuita eti ccmJamhuri!Viwanja vyote vya michezo nchini wamejitwalia kiharamu. Unatakiwa ifike mahali hizi mali zitaifishwe.
Inashindikana nini kutaifisha mali walizochuma watanzania pamoja, wakati ilikuwa rahisi kutaifisha shule za mashirika ya dini, au mkoloni mweusi anatisha kuliko mkoloni mweupe?
Ofisi gani hizo zinazojengwa na wanachama wa Chadema? Watu tumetoka kazini tumechoka wewe unaleta mizaha!CHADEMA wanajenga ofisi kwa nguvu za wanachama wao hivyo zitabaki kuwa za chama tofauti na CCM baadhi ya nyumba zao na viwanja vyote vya mpira na sabasaba vimejengwa kwa fedha za umma na rasilimali za serikali kama watumishi na vyombo vya ujenzi na pia wananchi wa kawaida na pia wafanyabiashara ambao wala si wanachama wao!
Pole kwa kazi! Ni vema ukawa unapata muda wa kutafuta habari!Ofisi gani hizo zinazojengwa na wanachama wa Chadema? Watu tumetoka kazini tumechoka wewe unaleta mizaha!