Mali za jide zazua kizaa zaa

Mali za jide zazua kizaa zaa

Hivi nyie wanawake aliyewalaani ni nani hasa?? Kila siku mnapiga kelele usawa usawa. 50 by 50.

Nyie hapo mnashabikia angekuwa jide mungeanza kelele.

Ebu jitbueni acheni unafiki.
We nae unaongea nini hata hueleweki,mara 50 by 50 mara laana, ungeazisha post yako kama umeguswa sana,ntoleee unafiki wako hapaa
 
Jambo limezua jambo! Siku chache baada ya kukabidhiwa talaka na aliyekuwa mumewe, Gardner G. Habash ‘Captain’, mali za mrembo wa nguvu, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ zinadaiwa kuzua kizaazaa baada ya kusemekana kutokea mvutano wa baadhi ya ndugu wa mwanamuziki huyo kutaka amgawie mtalaka wake huyo, Amani lina ubuyu kamili.

TUANZE NA TALAKA

Baada ya Jide au Lady Jaydee kuishi kwa zaidi ya miaka 9 ndani ya ndoa na Gardner, Februari 12, mwaka huu, wawili hao walivunja rasmi ndoa yao katika Mahakama ya Mwanzo Manzese- Sinza jijini Dar na kila mmoja kupewa hati yake ya talaka hivyo hadi leo zimepita siku 35 tangu walipotengana.

USTAWI WA JAMII WALIAMUA

Licha ya kupeana talaka, awali vikao vya ugawaji wa mali katika Idara ya Ustawi wa Jamii, Magomeni jijini Dar viliamua kuwa Gardner hakuwa na chake katika mali kwa kile kilichoelezwa kwamba, alikuwa kama mwajiriwa katika kazi za sanaa za Jide.
Mjengo wa Jide ulioko maeneo ya Kimala.

TWENDE KWA NDUGU WA JIDE

Ndugu wa Jide aliyejitambulisha kwa jina moja la Jack, aliliambia Amani kwamba, baadhi yao wamecharuka na kumwambia Jide atende haki kwa kumgawia mwenzake (Gardner) kwani hawana kinyongo naye na walimtambua kama mume kwa kipindi chote cha ndoa yao.
“Ni mvutano! Kuna ambao wanataka Jide agawe asilimia hamsini kwa hamsini ya mali zake kwa vile licha ya kwamba alikuwa kama meneja wake katika kazi, lakini kwa upande mwingine alikuwa ni baba wa familia. Lakini kwa upande wa ndugu wa Gardner, hatujasikia wakisema lolote.”

WENGINE HAWATAKI KUSIKIA

“Hata hivyo, kuna ambao hawataki kusikia Gardner anapewa hata senti tano kwani wanaamini ndugu yao (Jide) hana hatia hivyo Gardner ale jeuri yake maana alishindwa mwenyewe kuheshimu ndoa na kusababisha migogoro,” alisema ndugu huyo na kuongeza:

WATOLEANA MANENO MAKALI

“Hali imefika pabaya, imefika mahali wale ambao wanataka Jide asimpe chochote Gardner wanawapa maneno makali wale wanaotaka apewe. Kila mmoja anavutia kwake.”

KESI YATAJWA

Kwa mujibu wa chanzo chetu kingine cha habari, baadhi ya ndugu hawaridhiki na kizaazaa hicho hivyo kutaka kumshawishi Gardner akafungue madai ya mali mahakamani ambapo wanaamini atapata haki yake.
“Wamekasirika! Wanaona bora wamtafute Gardner wamuume sikio aende mahakamani,” kilisema chanzo hicho.

JIDE BIZE NA PROJEKTI MPYA

Wakati ndugu hao wakisigana hadi kutoleana maneno makali, imeelezwa kuwa Jide ‘ameziba’ masikio akiwa ameelekeza nguvu zake katika projekti yake mpya ya Naamka Tena.
“Wamempelekea taarifa za mvutano, Jide hataki hata kuwasikiliza. Yupo bize na projekti yake ya Naamka Tena, si unajua zimebaki siku chache arudi upya kwenye soko? Hawajibu kama atamgawia mali hizo au la,” kilisema chanzo.
Jide akiwa na mkoko wake aina ya Range Rover Evoque.

JIDE HUYU HAPA

Jitihada za Amani kutaka kujua undani wa habari hiyo ziligonga mwamba kufuatia simu ya Jide ya mkononi kuita bila kupokelewa.
Hata hivyo, Amani lilitumia njia ya meneja wake aliyeomba hifadhi ya jina na kufanikiwa kumpata Jide waliyekuwa naye pamoja ambapo alikiri kutokea kwa mvutano huo wa ndugu lakini akaomba aachwe kwani yupo bize na shughuli za ujio wake mpya.
“Jamani mvutano ni wa kawaida. Mimi nipo bize na ujio wangu mpya, mbona hamniulizi kuhusu kazi yangu mpya ya Naamka Tena? Kuhusu mali mimi naheshimu uamuzi wa Ustawi wa Jamii,” alisikika Jide.

GARDNER SASA

Baada ya kumalizana na Jide, Amani lilimgeukia Gardner, mtangazaji maarufu Bongo wa Redio EFM ili kumsikia anazungumziaje kuhusu mvutano huo wa mali na namna ambavyo baadhi ya ndugu wa Jide wanamtetea.
“Hivi kuna ndugu wana huruma hiyo? Mungu awabariki sana. Kwa upande wangu mimi namshukuru Mungu ni mzima wa afya, napambana kutafuta maisha yangu. Sina mpango wa kudai mali, najua Mungu atanipa tu,” alisema Gardner.
MALI ZENYEWE NI ZIPI?
Mali ambazo zipo mikononi mwa Jide hadi sasa ni pamoja na nyumba zilizopo Tegeta, Kimara-Temboni na Kiwalani jijini Dar. Pia kuna shamba (haikujulikana ekari ngapi) lililopo Bagamoyo, Pwani.
Gari aina ya Nissan Murano analo Jide, Range Rover Evoque analo Jide na basi lililokuwa likitumiwa kubebea vyombo na wanamuziki kwenye Bendi ya Machozi.
Hehehehehehehehhe mashabiki wa diamond mpo? ukitaka mwanaume kuolewa tii sharia za kuolewa na mwanamke au yatakukuta yalio kuta Gadina, wapo weng +++++++ Uganda oyeeeeeeeeeee mumeowa kaka yetu kesi Uganda heheheheheheheheeheheh
 
Kama hakufata pesa kwanini alikubali kumuacha mpenziwe wa kufa na kuzikana na kukubali kuolewa na jide, pesa zilimuoa.... asante jide aliona mbali kumbe.... alikuwa kama mfanyakazi wake na si mume, very smart jide,na kwa wanawake wengine wenye pesa nashauri kabla hawajaolewa na waume waliowazidi kifedha wasisahahu prenap agreement.... maana wanaume wengi hufata pesa huku wakiwa na wanaowapenda kweli nje ya ndoa,mwanaume simama utafute mwenyewe na si nyuma ya mgongo wa mkeo
Kwani kuzaa na mtu ni kumuoa? Hata hivyo mbona alipomuoa jide alikuwa hana kitu.
 
hivi miaka yote 9 Gardner tuseme hakuwahi kutoa idea yeyote hata ushauri wowote wa kimaendeleo kwa jide?
Yaani ni jambo la ajabu sana mimi nashindwa kuelewa hizi sheria za ndoa, hua zinafanya kazi kwa mwanaume tu? Maana najua angekua mwanaume ndiyo mwenye pesa tungeona kasheshe yake.
 
Hahahaa, alieanza kumquote mwingine nanii, unantishia paka mimi na choko umezianza mwenyewe, kwendraaa....
Nimekukwote kwa shari??? Zembwera mkubwa ebu nikaushie nakutishia nyau..! Toa kichwaa nikuponde.
 
hawa ndugu ndio wabaya wake hasa huyo jide,kama anakaa nao anatakiwa awafukuzilie mbali.
Hawa wana kinyongo na mafanikio yake na wanamchimba kumkomoa

Tena mkuu sio kinyongo cha mafanikio yake Jide tu nasema mbali ya kuwatimua kwake wala wanachopika kuanzia chai na chochote asile. Awe na sehemu tofauti ya kula wanaweza kumtoa hata roho au kuunguza jengo au lolote baya.Timua kabisa hawa tena wasivyo na chembe ya aibu wanampangia na asilimia ya kumpa Gardner. Wangekuwa wao wangetoa hata senti?
 
Hili suala liwe fundisho kubwa kwa vijana mliooa na mnaotarajia kuoa kwa kumilikisha kila kitu mwanamke kisa mnapendana. Mwanamke SIO NDUGU ni RAFIKI. Leo mpaka mzeeke. Ukimpa mpe. Usitegemee akupe mkigombana. Jifunzeni hilo.
 
kama kweli gardner alikuwa busy kuponda mali akipata mshahara hawekezi hata kidogo basi avune alichopanda .

ila kama alikuwa anachangia anachopata Jide hajafanya haki alikuwa mme wake endapo wamefanya wote hayo maendeleo asimwache mwenzie akaanze uoya jaman hiyo mijumba yote akimpa 1&gari 1 atapungukiwa nini? hana hata hofu ya mungu akajihisi dhulumati aiseee dahhh, labda kama gardner akipata kidogo kilikuwa kinaishia club dahh hadi huruma
 
Nimekukwote kwa shari??? Zembwera mkubwa ebu nikaushie nakutishia nyau..! Toa kichwaa nikuponde.
Kumbe sio kwa shari mbona povu linakutoka kama una degedege,nipishee.. Hebu kiponde tuone,mxeeew
 
Back
Top Bottom