Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Habari wakuu,
Wakati wa Mkapa ulitokea uuzaji wa nyumba za serikali, na kigezo cha kuweza kununua nyumba hizo ilikuwa uwe mtumishi wa serikali. Jamii iliona ni sawa na haki, lakini kumbe jambo sawa na la haki ilikuwa kwa watumishi hao kutoruhusiwa kabisa kununua nyumba zile.
Wanazuoni wanasema kuwa mali za Serikali zinapatikana kwa kupitia kodi, kwa hiyo hata wakati zinapouzwa ni haki wale walipa kodi ndiyo wakapewa nafasi ya kununua. Watumishi wa serikali, kuanzia Rais, mawaziri, wabunge na watumishi wengine wote wanaolipwa na serikali si walipa kodi bali ni watu wanaotumia kodi.
Si haki kumuuzia mtu ambaye hakuhusika kuchangia kupatikana mali hiyo huku ukimuondoa kabisa yule aliyehusika kuinunua. Kwa mantiki hiyo, mali yoyote ya Serikali inapouzwa, iwe nyumba, magari, viwanja, mashamba n.k, watumishi wa serikali hawapaswi kuruhusiwa kununua.
Nawasilisha.