Mkuu, kwa nini umeamua kuyasema yote haya bila kuwa na uhakika wa point unayoitetea?
Kifupi wafanyakazi wa serikali ni walipa kodi wazuri wasioweza kukwepa, tena kodi kubwa kubwa.
Ningelikuelewa kama ungelisema kuwa, wasipewe nafasi ya kununua mali hizo kwa sababu, wanaghushi ubovu wa vifaa na kujiuzia bei ya kutupwa, hapo ningeielewa context.
Nyumba, sijui magari nk nk vingi vizima hughushiwa ubovu ili waweze kujiuzia kwa bei ndogo.
Jambo jingine wanufaika katika minada hiyo ni wakubwa wenye vyeo huko makazini, lakini mtumishi wa chini mpaka akauziwe, jua kazunguka mbuyu!
Wangelipigwa marufuku kujiuzia mali hizo wao, basi minada hiyo ingelikuwa ya haki na manufaa, si kwa serikali tu bali kwa umma.