Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kukamata TV, Redio na Laptops zenye thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 30 ambazo Wahalifu waliziiba maeneo ya Kigamboni na tayari vitu hivyo vimetambuliwa na Wamiliki wake.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es saalam, Muliro Jumanne amesema ukamataji huo umefanikiwa kutokana na operesheni kali iliyoendeshwa usiku na mchana katika Wilaya zote za Dar es salaam.
Muliro amesema “Operesehni hii maalum imeanza June 12 na mpaka sasa ina mwezi mmoja, katika operesheni hii kali baadhi ya Watu wamesalimisha silaha maeneo ya Chamanzi”