Maliasili na Utalii Yapongezwa kwa Kutafsiri Maono ya Rais Samia

Maliasili na Utalii Yapongezwa kwa Kutafsiri Maono ya Rais Samia

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.31.jpeg

Wizara ya maliasili na utalii imepongezwa kwa kutafsiri kwa vitendo maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha juhudi kubwa katika kuendeleza sekta ya utalii kwa kufanya uwekezaji mkubwa kwenye Taasisi za wizara ikiwemo Mamlaka ya usimamizi wa Wanyapori Tanzania (TAWA).

Pongezi hizo zimetolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, wakati wa kuhitimisha ziara ya ukaguzi wa Miradi inayotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori katika (TAWA) katika Hifadhi ya wanyamapori Makuyuni.

WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.32 (1).jpeg


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma imeongeza kuwa iko haja kwa Taasisi zilizokabidhiwa maeneo yaliyotaifishwa na serikali kuja kujifunza katika eneo la Hifadhi ya wanyamapori Makuyuni juu ya uwekezaji na uendelezaji uliofanywa na TAWA kwa kipindi kifupi baada ya kukabidhiwa eneo hilo kutoka kwa Msajili wa Hazina.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma imefanya ziara katika hifadhi ya Wanyamapori Makuyuni kwa lengo la kukagua utelezaji wa miradi na uendelezaji wa eneo hilo baada ya kukabidhiwa kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kutoka kwa Msajili wa Hazina baada ya kutaifishwa kutoka kampuni ya Rift Valley Seed Company Limited,

WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.33 (1).jpeg


Baada ya kukabiidhiwa eneo hilo, TAWA walilifanya kuwa Hifadhi ya Wanyamapori na kuwekeza katika kuboresha miundombinu ili kuvutia watalii ambapo tangu likabidhiwe mwezi machi 2023, idadi ya watalii waliotembelea imeongezeka kutoka 291 mwaka 2023/24 hadi 405 kwa kipindi cha Julai 2024 – Januari 2025; lakini pia ukusanyaji wa mapato uliongezeka kutoka Shilingi 14,535,832.08 mwaka 2023/24 hadi Shilingi 251,655,828.28 katika kipindi cha Julai 2024 hadi Januari 2025.

Naibu Waziri Maliasili na Utalii, Mhe Dunstan Kitandula aliishukuru kamati kwa kuona umuhimu wa kuja kuona kwa uhalisia uendelezaji na uwekezaji mkubwa unaondelea kufanywa na wizara kupitia TAWA, Vilevile alisema kuwa muonekano wa eneo hilo kwa sasa ni maono ya Mhe. Rais katika kuendeleza sekta ya utalii lakini pia ni ushauri unaotolewa na wabunge kupitia michango yao mbalimbali katika Sekta ya Utalii.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.32.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.32.jpeg
    84.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.33.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.33.jpeg
    100.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.34 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.34 (1).jpeg
    118 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.36.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.36.jpeg
    129.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.37.jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.37.jpeg
    100.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.37 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.37 (1).jpeg
    125.1 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.38 (1).jpeg
    WhatsApp Image 2025-02-10 at 11.25.38 (1).jpeg
    76.2 KB · Views: 2
Back
Top Bottom