Malinyi, Morogoro: Joanfaith Kataraia atunukiwa ngao ya Ushindi kwa Kuongoza katika Ufaulu PSLE. Nini kipo nyuma ya mafanikio ya DED huyu?

Malinyi, Morogoro: Joanfaith Kataraia atunukiwa ngao ya Ushindi kwa Kuongoza katika Ufaulu PSLE. Nini kipo nyuma ya mafanikio ya DED huyu?

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029
E53L6QhBDNBRJWAaeLQQeHTF.jpg

Hebu tujadili kwa pamoja, nini kipo nyuma ya mafanikio haya makubwa ya Mhe Joanfaith Kataraia Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Malinyi,tangu kuteuliwa kwake wakati wote ameongoza kwa Ufaulu wa juu kwenye mitihani ya ,PSLE,pamoja na mambo mengine mbalimbali,

==
Mhe Joanfaith akiwa katika hafla ya kukabidhiwa "Tuzo" yake ya heshima (certificate of appreciation) kama mkurugenzi mtendaji bora wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi anahaya ya kusema,

eSPMaCF96g0J45AyNKX261t4.jpg

" Halmashauri yangu ya Malinyi imekuwa ikiongeza kiasi cha ufaulu kwenye mitihani yote ya kuhitimu Elimu ya Msingi (PSLE) kwa miaka mitatu mfululizo tangu 2019|2020 hadi 2021|22 kwa mchanganuo ufatao;

Mwaka 2019|20 , Wilaya ya Malinyi tulishika nafasi ya pili ( 2 ) Kimkoa (Morogoro) na nafasi ya 43 Kitaifa kwa Ufaulu wa 89.17 %

Mwaka 2020|21, Wilaya ya Malinyi tulishika nafasi ya 1 Kimkoa (morogoro) na ya 9 Kitaifa kwa ufaulu wa 96.03 %

Mwaka 2021|22, Malinyi tulishika nafasi ya kwanza Kimkoa (morogoro) na nafasi ya kumi (10) Kitaifa kwa ufaulu wa 96.06%

Mhe Joanfaith Kataraia anasema, Halmashauri ya wilaya ya Malinyi imejipanga kuendelea kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji darasani pia kwa vitendo ili wakati wote kupata matokeo ya juu kimkoa na Kitaifa,

Kwanza, tunaimarisha ufundishaji wa stadi za kusoma,kuandika na kuhesabu.

Pili,tunatoa motisha kwa walimu na kulipa stahiki zao kwa wakati.

Tatu, tunashirikiana na viongozi wa Serikali za Vijiji na Wazazi kudhibiti Utoro mashuleni.

Nne, tunaendelea kuboresha Miundombinu ikiwemo Madarasa,Matundu ya vyoo,Madawati na nyumba za Walimu.

Tano, tunashirikiana na wadau wa elimu kuinua ufaulu na kuboresha miundombinu ya Kujifunzia na kufundishia,

Mhe Joanfaith anaendelea kusema, Tunamshukuru mkuu wetu wa Mkoa Mhe Martine Shigela pamoja na Mkuu wetu wa Wilaya Mhe Mathayo Masele kwa ushirikiano wao katika kupata matokeo haya ya juu kabisa kimkoa na Kitaifa,

Anaendelea kusema, Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Tunamshukuru zaidi Mheshimiwa Rais,Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Upendo wake kutufanyia yafuatayo :-

•√ Kuendelea kuajiri Walimu wa kutosha,

•√ Kutoa Elimu bila Malipo kuanzia chekechea mpaka kidato cha sita,

•√ Kutoa fedha za ujenzi wa matundu ya vyoo karibu katika kila shule,

•√ Kutoa fedha nyingi za ujenzi wa vyumba vya madarasa.

•√ Kutoa fedha za ujenzi wa shule za msingi mpya.

•√ Kutoa fedha za ujenzi wa nyumba za waalimu.

•√ Kutoa fedha za kufanikisha shughuli za mitihani.

•√ Kutoa fedha za mradi wa kuimarisha ujifunzaji wa elimu ya awali na Msingi.

SHIRIKI KIKAMILIFU SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2022 KWA MAENDELEO ENDELEVU YA TANZANIA.🇹🇿🇹🇿🇹🇿

Jiandae Kuhesabiwa..
 
Hongera Sana DED

👇👇👇👇👇👇

=>Huyu mkurugenzi anabidii Sana ya kazi,

=>Ni mchamungu Sana

=> Yuko social na kila mtu

=> Anajali Sana watumishi wake

=>She is also beautiful ila haringi,

=>Wengine wenye madaraka jifunzeni kwa huyu binti,


Niliwahi kuandika hii kabla ya hii TUZO,


👇👇👇👇👇


 
Kuna wanafunzi kibao waliofaulu darasa la saba kwenda kidato cha kwanza ambao kusoma kiswahili tu ni shida halafu huyu DED anapongezwa, hii nchi sijui inakwenda wapi. Haya ndio madhara ya kufikiri kwamba UPINZANI ni uadui nchini, huu upuuzi unaoitwa kuupiga mwingi sishani kama ungekuwepo kama upinzani active ungekuwepo
 
Kuna wanafunzi kibao waliofaulu darasa la saba kwenda kidato cha kwanza ambao kusoma kiswahili tu ni shida halafu huyu DED anapongezwa,hii nchi sijui inakwenda wapi.Haya ndio madhara ya kufikiri kwamba UPINZANI ni uadui nchini,huu upuuzi unaoitwa kuupiga mwingi sishani kama ungekuwepo kama upinzani active ungekuwepo
Huu utafiti umeufanya Shule gani kiongozi?
Tangu lini Tanzania ikawa na Upinzani?


Mimi ni CHADEMA ila naipenda CCM
 

Joanfaith Kataraia atunukiwa ngao ya Ushindi kwa Kuongoza katika Ufaulu PSLE. Nini kipo nyuma ya mafanikio ya DED huyu tangu kuteuliwa kwake?​



👆👆👆👆


Atakuwa anamtegemea Mungu na kufanya kazi kwa bidii
 

Joanfaith Kataraia atunukiwa ngao ya Ushindi kwa Kuongoza katika Ufaulu PSLE. Nini kipo nyuma ya mafanikio ya DED huyu tangu kuteuliwa kwake?​



👆👆👆👆


Atakuwa anamtegemea Mungu na kufanya kazi kwa bidii
 
Joanfaith,

1. Sura nzuri ✔️

2. Elimu nzuri ✔️

3. Matokeo mazuri PSLE ✔️

4. Mchamungu mzuri ✔️

5. Mtu wa watu ✔️

Huyu anapashwa kupewa nafasi ya juu kwa maslahi ya Watanzania
 
Hongera Sana DED

👇👇👇👇👇👇

=>Huyu mkurugenzi anabidii Sana ya kazi,

=>Ni mchamungu Sana

=> Yuko social na kila mtu

=> Anajali Sana watumishi wake

=>She is also beautiful ila haringi,

=>Wengine wenye madaraka jifunzeni kwa huyu binti,


Niliwahi kuandika hii kabla ya hii TUZO,


👇👇👇👇👇


Uko vizuri ila hama icho chama unajichelewesha Sana
 
Back
Top Bottom