Malinzi na Mwesigwa waendelea kuzoeshwa maisha ya kuishi Segerea

Malinzi na Mwesigwa waendelea kuzoeshwa maisha ya kuishi Segerea

uchguzi upite au ajitoe huko huko jela hawezi kugombea nafas yoyote lasivyo ataoza.
 
hivi huyu mwanae si mtangazaji wa clouds kipindi cha ala za roho?
 
MALINZI AGONGA TENA MWAMBA KISUTU ,AREJESHWA RUMANDE MPAKA JULAI 30

Dar Es Salaam,Tanzania.

KESI inayomkabiri Rais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi,Katibu wake Celestine Mwesigwa na Mtunza Fedha,Nsiande Mwanga imesoma tena leo asubuhi kwenye mahakama ya Kisutu,Dar Es Salaam.

Imeamuliwa kuwa Malinzi pamoja na wenzake warejeshwe tena rumande kwa madai kuwa upelelezi wa kesi yao bado haujakamilika na watarejeshwa tena mahakamani hapo Julai 30 mwaka huu.

Malinzi anakabiriwa na mashitaka 28 ya kughushi nyaraka na kutakatisha fedha wakati Mwesigwa na Mwanga wanakabiriwa na mashitaka matatu kila mmoja.

Malinzi na wenzake walifikishwa kwenye mahakama ya Kisutu kwa mara ya kwanza Juni 29 kabla ya kupandishwa tena kizimbani Julai 3 mwaka huu.
NI JULY 31 MKUU....EDIT POST YAKO
 
Malinzi kama atapigia tena kampeni CCM basi ana laana ya wazazi.

Kwani nani kakuambia kuwa hata akitoka huko ' Segerea ' bado atakuwa tena ni Rais wa TFF? Tayari tumeshaanza kujiandaa kumshangilia Rais mpya wa TFF Ally Mayai na Makamu wake Mtemi Ramadhan na huyo Malinzi wako labda kampeleke akawe Rais wa Familia yako.

Tayari ' Mission Accomplished ' na alionywa mapema tu akajifanya Yeye ni ' Kiburi ' sasa yamemkuta na akifanya mzaha ' ataozea ' Segadansi hata maisha.
 
kweli upelelezi bado au uchaguzi upite

Kwani tulivyosema mwanzo juu ya ' Umafia ' huu wa kuzidi kumuweka ndani ' makusudically ' hadi ' Uchaguzi ' Mkuu wa TFF upite hamkutuelewa? Halafu nilishasema kuwa Malinzi aache ' Kiburi ' kwani anachotakiwa kufanya ili atoke hata kwa ' dhamana ' ni jambo dogo mno nalo ni ' Kutangaza ' tu kupitia ' Wakili ' wake kuwa ameamua rasmi kuachana na TFF na masuala ya Mpira wa Miguu Tanzania. Hili nililisema mapema tu lakini anajifanya bado ' anadinda / anabisha ' sasa ngoja azidi kuonyeshwa ' Umafia ' na System.
 
hivi huyu mwanae si mtangazaji wa clouds kipindi cha ala za roho?

Hapana Mkuu bali ni ' Bao ' la ' Ujanani ' kwa Kaka yake yule ambaye nae pia ' katimuliwa ' kule BMT.
 
Wacha wasote tu maana hamna namna walikula kivulini zamu yao kulia juani
 
Kwani nani kakuambia kuwa hata akitoka huko ' Segerea ' bado atakuwa tena ni Rais wa TFF? Tayari tumeshaanza kujiandaa kumshangilia Rais mpya wa TFF Ally Mayai na Makamu wake Mtemi Ramadhan na huyo Malinzi wako labda kampeleke akawe Rais wa Familia yako.

Tayari ' Mission Accomplished ' na alionywa mapema tu akajifanya Yeye ni ' Kiburi ' sasa yamemkuta na akifanya mzaha ' ataozea ' Segadansi hata maisha.
Wapi nimesema akitoka atakuwa Rais TFF
 
Hapa CCM imeingiaje tena Mkuu? Kwani alipokuwa ' akiiba ' alikuwa akila na Watu wa CCM? Hivi kweli Mtu aliye ' makini ' kabisa anaweza kulihusisha hili suala la ' Upuuzi ' wa Malinzi na CCM?
Wewe uliye makini unalihusisha na nini?
 
Muda mchache uliopita Viongozi wa TFF Rais Jamal Emil Malinzi na Katibu Mkuu wake Celestine Mwesigwa wamerudishwa tena Segerea hadi tarehe 31 mwezi huu ambapo Kesi yao itatajwa tena baada ya upande wa Washtaki kukataa ombi la Mawakili wa hawa Viongozi.

Nawasilisha.
Kwani haki ya dhamana inatolewa kwa ridhaa ya washitaki au hoja za kisheria??

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Kabla hujajianika ulivyo mweupe kichwani na kila mtu kukuona mjinga Jaribu kujielimisha kwanza, kesi za money laundering (utakatishaji pesa) hazina dhamana.
Umejuaje kuwa ni kesi ya "money laundering" kungali hapana ushahidi?? Sheria zetu zina naksi.

Huyo anayeshitaki anatakiwa warau aonesha preliminary proof kwamba kuna aina hiyo ya kosa amelifanya mtuhumiwa.

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom