Malipo kwa Dola badala ya Shilingi yanaongezeka Mitaani, Serikali iko kimya

Malipo kwa Dola badala ya Shilingi yanaongezeka Mitaani, Serikali iko kimya

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Niende moja kwa moja kwenye wazo langu. Licha ya kwamba biashara ni huria lakini naamini Nchi ina taratibu zake hasa kwenye masuala ya Kifedha. Na imeshatokea mara kadhaa Serikali kuagiza malipo ya ndani ya Nchi isipokuwa kwa Watalii yafanyike kwa Shilingi ya Tanzania lakini hali ni tofauti.

Ukienda kupata huduma nyingi siku hizi ikiwemo katika baadhi ya taasisi za Umma wanakutaka ulipe kwa Dola nashindwa kuelewa sababu ni uhaba wa Dola au ndio kukosa udhibiti wa Kifedha?

Kuendelea kuruhusu hali hii ndio chanzo cha kuzorotesha thamani ya Tsh. dhidi ya Dola. Sijajua Serikali inapanga nini kwenye hili.

Soma zaidi Serikali yang'ang'ania malipo kwa dola
 
Toa mifano ya hizo taasisi la sivyo huu utakuwa umbea na uzushi.
 
Ukienda kupata huduma nyingi siku hizi ikiwemo katika baadhi ya taasisi za Umma wanakutaka ulipe kwa Dola
Taja ni taasisi gani wanapokulazimisha ulipie Dola? Acha porojo
 
Back
Top Bottom