Malipo ya 500/= getini stendi ya Magufuli magari madogo yanayotoka na abiria;

Karungikana

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2017
Posts
913
Reaction score
844
Nimeshangazwa sana na malipo yanayotozwa getini stendi ya Magufuli, kwa magari madogo yaliyobeba abiria walioshuka kwenye mabasi.

Kuna jamaa getini anachukua mia tano kwa kila gari ndogo inayotoka, bila kutoa risiti, na mlipaji ni abiria. Hizo pesa zinaishia wapi na ni tozo za sababu gani?
 
Nchi hii kila mtu anakula sehemu yake

Ila ndani ya stendi kulipia inakuwaga kawaida sema kwanini hawatoi risiti

Ova
 
Hujadai risiti hata ya mchongo? Ungekomaa kudai risiti ndio ungepata picha halisi..
 
Ana familia muache aokote chochote kitu Mkuu.

SIKU NYENGINE KATAA MPAKA AKUPE RISITI.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Hivi mabasi yanapitaga vituo vile kufanya nini kila yanapoingia mkoa flani
 
Nchi hii kila mtu anakula sehemu yake

Ila ndani ya stendi kulipia inakuwaga kawaida sema kwanini hawatoi risiti

Ova
Nasikia pia vyoo vya stand za mabasi viko vizuri zaidi ya vyoo vya Airport Mkuu.
Maana bila pesa haujisaidii 🤣 😂😂
 
Hujadai risiti hata ya mchongo? Ungekomaa kudai risiti ndio ungepata picha halisi..
Nilikazana sana kudai risiti, hakuwa nazo. Pamoja na uchovu wa safari, nikaona wacha tu nijiendee nyumbani.
 
Back
Top Bottom