<div class="bbWrapper"></div>
- Tunachokijua
- TANESCO ni shirika la umeme Tanzania lenye wajibu wa kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme kwa wananchi.
Madai
Mdau wa JamiiCheck.com amehitaji kupata ualisia iwapo ni kweli TANESCO wanakusanya namba za mita na majina ya wamiliki wakidai mapato hayo yanataka kuondolewa na kurudishwa katika halmashauri.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa si ya kweli. JamiiCheck imewasiliana na TANESCO kupitia kwa Mkurugenzi wa Uhusiano kwa Umma, Irene Stanley ambaye amekanusha kuhusu suala hilo na kuwataka wananchi kuwa makini kwa kutokutoa Taarifa.
"Hiyo taarifa haina ukweli wowote, ni uongo, Wananchi wawe makini wasitoe taarifa zozote za LUKU kwani TANESCO tunao mfumo unaomtambua mtumiaji moja kwa moja." - Irene Stanley