Wapo vijana wanaopita mitaani wanaodai wametumwa na serikali za mitaa, kwa lengo kuchukuwa namba za luku za kila mita na majina ya wamiliki, wakidai mapato hayo yanataka kuondolewa na kurudishwa katika halmashauri, je hili ni la kweli?
Ushauri wangu kama ni la kweli, je kwanini mapato hayo ambayo yanakusanywa na TANESCO kila mwisho wa mwezi yasihamishiwe moja kwa moja katika halmashauri, badala ya kutaka kuvuruga mfumo safi uliopo?
Ushauri wangu kama ni la kweli, je kwanini mapato hayo ambayo yanakusanywa na TANESCO kila mwisho wa mwezi yasihamishiwe moja kwa moja katika halmashauri, badala ya kutaka kuvuruga mfumo safi uliopo?
- Tunachokijua
- TANESCO ni shirika la umeme Tanzania lenye wajibu wa kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme kwa wananchi.
Madai
Mdau wa JamiiCheck.com amehitaji kupata ualisia iwapo ni kweli TANESCO wanakusanya namba za mita na majina ya wamiliki wakidai mapato hayo yanataka kuondolewa na kurudishwa katika halmashauri.
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia madai hayo na kubaini kuwa si ya kweli. JamiiCheck imewasiliana na TANESCO kupitia kwa Mkurugenzi wa Uhusiano kwa Umma, Irene Stanley ambaye amekanusha kuhusu suala hilo na kuwataka wananchi kuwa makini kwa kutokutoa Taarifa.
"Hiyo taarifa haina ukweli wowote, ni uongo, Wananchi wawe makini wasitoe taarifa zozote za LUKU kwani TANESCO tunao mfumo unaomtambua mtumiaji moja kwa moja." - Irene Stanley