Malipo ya viwanja

Malipo ya viwanja

MAKINYA

Senior Member
Joined
Dec 20, 2012
Posts
139
Reaction score
54
Naomba ufafanuzi kwa anayefahamu

1. Namna gani bei za kulipia viwanja halmashauri zinakokotolewa, na wapi au sheria ipi wanaitumia kupata gharama kamili. Kwakweli nimetatizwa na kiwango kilichotolewa na halmashauri moja hapa nchini juu ya malipo wanayotakiwa kulipa watu waloomba viwanja vilivyotangazwa, mathalani fomu ya kuomba kiwanja kimoja ilikuwa inalipiwa elfu themanini.

Majina yametoka kwa mfano mtu alopata kiwanja (SLD) ENEO LENYE MSONGAMANO MDOGO, anatakiwa kulipa shilingi milioni nne elfu arobaini na mia tisa (4,040,900). Tangazo limetolewa tarehe 25.05.2013, halafu mwisho wa kulipia ni tarehe 12.06.2013.

Hapo nimetoa mfano wa kiwango cha kati lakini wapo watu wanatakiwa kulipa hadi milioni 17, sasa sijui hata kama ni halali kwa Mtanzania wa kawaida anawezaje kupata fedha yote hii kwa kipindi kifupi namana hii?

Nawasilisha hoja.
 
Fomu ya maombi iko kwa mujibu wa sheria inaitwa land form no 19 malipo yake inategemea halmashauri husika ilivyopanga in most cases halmashauri nyingi zinachaji elfu kumi,malipo mengine ni gharama za kiwanja kama premium kulingana na rate ya kuuzia mita moja ya mraba ya ardhi kutokana na matumizi ya ardh husika, gharama za upimaji na ramani pamoja na gharama za umiliki kama utayarishaji wa hati, kodi ya ardhi, usajili wa hati, stamp duty ambazo zipo kwa mujibu wa sheria.
 
Hili jambo limeniokoa sana wadau, asanteni sana, nlikua natafuta uelewa husu hili jambo.
Fomu ya maombi iko kwa mujibu wa sheria inaitwa land form no 19 malipo yake inategemea halmashauri husika ilivyopanga in most cases halmashauri nyingi zinachaji elfu kumi,malipo mengine ni gharama za kiwanja kama premium kulingana na rate ya kuuzia mita moja ya mraba ya ardhi kutokana na matumizi ya ardh husika,gharama za upimaji na ramani pamoja na gharama za umiliki kama utayarishaji wa hati,kodi ya ardhi,usajili wa hati,stamp duty ambazo zipo kwa mujibu wa sheria.
 
Back
Top Bottom