Naomba ufafanuzi kwa anayefahamu
1. Namna gani bei za kulipia viwanja halmashauri zinakokotolewa, na wapi au sheria ipi wanaitumia kupata gharama kamili. Kwakweli nimetatizwa na kiwango kilichotolewa na halmashauri moja hapa nchini juu ya malipo wanayotakiwa kulipa watu waloomba viwanja vilivyotangazwa, mathalani fomu ya kuomba kiwanja kimoja ilikuwa inalipiwa elfu themanini.
Majina yametoka kwa mfano mtu alopata kiwanja (SLD) ENEO LENYE MSONGAMANO MDOGO, anatakiwa kulipa shilingi milioni nne elfu arobaini na mia tisa (4,040,900). Tangazo limetolewa tarehe 25.05.2013, halafu mwisho wa kulipia ni tarehe 12.06.2013.
Hapo nimetoa mfano wa kiwango cha kati lakini wapo watu wanatakiwa kulipa hadi milioni 17, sasa sijui hata kama ni halali kwa Mtanzania wa kawaida anawezaje kupata fedha yote hii kwa kipindi kifupi namana hii?
Nawasilisha hoja.