Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limemuachia kwa dhamana Godlisten Malisa majira ya Saa saba Usiku wa kuamkia leo Juni 8, 2024.
Baada ya kuachiwa moja kwa moja yeye na wawakilishi wake wakiongozwa na Wakili Hekima Mwasipu wakaelekea Hospitali ya KCMC kutokana na afya ya Malisa kudaiwa kutokuwa nzuri.
Imeelezwa kuanzia jana Malisa amekuwa akilalamika kuwa anaumwa.
Wakili Hekima Mwasipu amesema wamesaini Bondi ya Milioni 10 na anatakiwa kumrejesha kituoni hapo saa tatu Asubuhi ya leo Juni 8, 2024.
============
AWALI ilikuwa hivi:
============
Wakili Kibatala: Malisa hajapewa dhamana, amehojiwa mara mbili, tunasubiri ahojiwe mara ya tatu
Wakili Peter Patience Kibatala amezungumzia suala linalohusu Godlisten Malisa kwa kuchambua kinachoendelea tangu alipokamatwa akiwa Mahakamani Dar es Salaam kisha kusafirishwa hadi Mkoani Kilimanjaro.
Anaelezea alivyokamatwa
Jana (Juni 7, 2024) nikiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu pamoja na Wakili Hekima Mwasipu tulikuwa katika majukumu ya kusimamia kesi inayowahusu Godlisten Malisa na Boniface Jacob kuhusiana na maandishi fulani yanayowahusu.
Mchakato uliokuwa unafanyika ni “Usikilizaji wa Awali Mahakamani” kwa lengo la kutambua mambo yanayobishaniwa dhidi ya mambo ambayo hayabishawini, kwa sababu kadhaa kesi hiyo ikahirishwa na kupangiwa tarehe nyingine.
Suala lilipomalizika, nikaendelea na majukumu yangu mengine, wakati wateja wangu wanatoka wakiwa ndani ya korido za Mahakama, akajitokeza Askari akajitambulisha na kumuweka chini ya ulinzi Malisa akisema anatuhuma zinazomkabili Mkoani Kilimanjaro na hivyo anatakiwa kuondoka naye.
Alalamika Malisa kukamatwa korido za Mahakamani
Kitendo hicho cha kukamatwa katika korido za Mahakama ni kitu cha kusikitisha, nakumbuka Tundu Lissu alishawahi kukamatwa katika korodo za Mahakama kama hivyo.
Nakumbuka pia kuna muongozo ulitolewa kuwa watu hawatakiwi kukaatwa kwenye korodo ili kuheshimu Mahakama, kaa kuna ulazima wa kuwekwa chini ya ulinzi basi wafanye hivyo nje ya Mahakama kwa maana ya kuheshimu eneo hilo la Mahakama.
Nilipoitwa na kujiridhisha kuwa waliomuweka chini ya ulinzi Malisa ni Askari nikaruhusu aende nao, wakati huohuo Wakili Hekima Mwasipu naye akaanza safari ya kwenda Moshi kwa kuwa walitueleza wanapoelekea.
Hakukuwa na haja ya wao kumfuata Mahakamani, kwani wanajua kabisa lazima aende Mahakamani na wangeweza kumpigia simu aende au kumjulisha mapema.
Malisa kuhojiwa
Usiku huo kuamkia leo (Juni 7, 2024), Malisa amehojiwa chini ya Wakili Hekima Mwasipu, baada ya hapo baadaye mchana akahojiwa tena mara ya pili.
Mahojiano ya mara ya kwanza yanahusu suala lake linalohusu anayedaiwa kuwa ni Mtumishi wa Profesa Adolf Mkenda (Waziri wa Elimu), mara ya pili akahojiwa kuhusu suala linalomhusu Mwalimu anayedaiwa alimuadhibu mtoto hadi akapoteza maisha.
Kuhojiwa mara ya tatu
Kuhusu dhamana hajapewa kwa maelezo kuwa kuna Maafisa wengine wa Usalama wanatarajia kuwasili leo kutoka Makao Makuu, tumeelezwa wanatarajiwa kumuhoji kuhusu suala lingine ambalo hatujaelezwa kuwa linahusu nini.
Pamoja na uwepo wa Wakili Mwasipu pia kuna Wakili mwingine ambaye naye anashiriki kumsimamia Malisa, anaitwa Shecky Mfinanga kutoka Arusha, pia kuna Wakili mwingine wa palepale Moshi.
Afya ya Malisa
Kuhusu afya ya Malisa ipo salama, anaendelea vizuri na mwenyewe anasema tuhuma hizo zimehamishiwa Moshi eneo ambalo anatarajiwa kuwania ubunge.