PostGE2025 Malisa: Hakuna Mtu au Taasisi inayoweza kuhonga mamilioni ya vijana nchi nzima. Kama ilifanyika Vyombo vya Ulinzi ni DHAIFU

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Anandika Godlisten Malisa...

​

"Mimi binafsi siamini kama vijana walihongwa. Hakuna mtu wala taasisi inayoweza kuhonga mamilioni ya vijana nchi nzima.

"Na kama ilifanyika hivyo basi vyombo vya ulinzi ni dhaifu. Kama yupo mtu anaweza kuhonga vijana nchi nzima na vyombo vya ulinzi visijue mpaka maafa yatokee, tafsiri yake ni kwamba vyombo vya ulinzi ni dhaifu. Lakini siamini kama vyombo vyetu ni dhaifu kiasi hicho. Vijana huwa wanasema ukitaka kujua polisi wapo serious subiri wawe wanakutafuta wewe.

"Kwahiyo kama kuna watu walihongwa polisi wangeshajua mapema na kuwakamata. Wangehongwa wawili, watatu labda wangelinda siri, lakini kuhonga nchi nzima na polisi wasijue ni ngumu kuamini.

"Sehemu kubwa ya vijana walioandamana walikua na madai yao ya msingi. Wapo waliokua wanapinga vitendo vya utekaji. Hawa ni watu waliopoteza ndugu zao, watoto wao au wazazi wao na hawajaona hatua zikichukuliwa kupata haki. Kwa mfano ndugu wa mzee Kibao walioshuhudia baba yao akishushwa kwenye basi na kwenda kuuawa kikatili, hivi wanahitaji kulipwa ili waandamane? Ndugu wa Soka, Mdude, Polepole, Ben Sanane na wengine je?

"Pili, vijana wamedai Tume huru ya uchaguzi na Katiba mpya kwa muda mrefu. Wanataka sauti zao zisikike kwenye sanduku la kura. Lakini wameshuhudia wasimamizi wakitiki kura vituoni na kuziweka kwenye masanduku. Yani msimamizi mmoja anatiki ballot paper 20 anazishindilia kwenye sanduku. Hivi wafuasi wa vyama vilivyoshiriki uchaguzi wakiona hivyo watasubiri kulipwa ili waandamane?

"Mtaani kuna mamilioni ya vijana waliohitimu ngazi mbalimbali za elimu lakini hawana ajira. Wachache walioamua kujiajiri wamekutana na vikwazo vingi vya kimfumo. Leo si ajabu kumkuta graduate anatembeza karanga barabarani na bado mgambo wa jiji watambugudhi na kumwaga karanga zake. Inauma sana. Kijana kama huyu hatasubiri kulipwa ili kuingia barabarani.

"Kesi za kusingiziwa, Tuhuma za ufisadi serikalini, kuminywa kwa uhuru wa maoni, Nepotism ni miongoni mwa mambo yaliyofanya vijana kuingia barabarani ili kupaza sauti zao baada ya kuona wamelalamika kwa muda mrefu bila kusikilizwa. Siamini kama walillipwa.!"

Uko na la kusema tofauti na point za Malisa?
 
Halafu maandamano yangekuwa yameratibiwa na mfadhili mmoja maana yake uharibifu ungekuwa wa kufanana nchi nzima sababu angewapa na script moja.

Kuna maeneo kulikuwa na mtiti ila vituo vya mafuta havijaguswa kabisa tena huyo Lake Oil anavyo viwili pale Kahama.
 
Nadhani washauri/informer wake wanamlisha matango pori ! Kila siku anakuja na sababu mpya !
 
vichwa ndezi mnaotetea udhalimu, hebu pumzisheni hivyo vidole na vichwa vyenu. Njaa huwa ipo tu hadi tunakufa haiishi, msiponzwe na shibe ya siku 2
 
Ndiyo michezo aliyoizoea yeye. Anahonga baiskeli, pikipiki, cash, etc.
 
Jeshi imara ila halikuwa na taarifa kuna vijana toka nje ya nchi wameingia nchini kufanya vurugu, if that's true at all. Sijui wanalinda nini? Smh
 
Kiukweli huyu kiongozi wetu anameza kila kitu anakua kama kasuku ubongo wake unashidwa kuchuja mambo
 
Walipanga foleni kama bodaboda wanaojaziwa mafuta kwenye kampeni za CCM?

Waliingiziwa kupitia miamala ya simu? Na kama ndio hivyo wana usalama walikuwa wapi?

Au ndio sababu ya .... Ionekene wananchi hawamtaki mkuu wa CCM.

Mimi ni mwalimu na sitakiwi kujihusisha na siasa.
 
Kama watu kuandamana kudai tume huru ya uchaguzi walilipwa kwanini serikali haikuwalipa watu wasiandamane pia?

Na je nani aliwalipa wapiga risasi kuua watu 10000+? au wanaharakati ndio walizilipa AK -47 zikaanza kufuata watu mitaani zinajifyatua?

Nani aliwalipa walioficha miili ya waliopigwa risasi na ndugu zao hawajawapata miili yao hadi leo?
 
1)walitoka nje ya nchi,hawakuwa watanzania/watanganyika
2)walifuata mkumbo,watanzania/watanganyika
3)walilipwa,

Sasa sijui la kweli ni lipi,na haya yote wakati yanatokea serikali na machinery zake zilikuwa wapi?Je kama nchi tuko salama kweli?
 
Dah hii nchi ina siri sana aisee, kumbe waandamanaji wenzangu mlinizunguka mkaenda kulipwa bhana 😭

Lamomy hadi ww babe
Babe was necessary? 😹😹

Okay, iko hivi “Mfa maji haiishi kutapatapa”
Bado hawajasema, ipo siku atayaongea yote yaliyo nyuma ya pazia.

Damu ya mtu haiendi bure!!
 
Mama haeleweki.
Mwanzo alisema ni vijana wanaotoka nje ya nchi ndo waliondama.
Sasa hivi anasema waandamaji walilipa pesa waandamane.
Mama angalia chanzo Cha kujikwaa usiangalie ulipo dondokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…