Voltaire
JF-Expert Member
- Sep 1, 2013
- 1,964
- 2,192
Ccm imetutawala anzia 61 to date!Anandika Godlisten Malisa...
"Mimi binafsi siamini kama vijana walihongwa. Hakuna mtu wala taasisi inayoweza kuhonga mamilioni ya vijana nchi nzima.
"Na kama ilifanyika hivyo basi vyombo vya ulinzi ni dhaifu. Kama yupo mtu anaweza kuhonga vijana nchi nzima na vyombo vya ulinzi visijue mpaka maafa yatokee, tafsiri yake ni kwamba vyombo vya ulinzi ni dhaifu. Lakini siamini kama vyombo vyetu ni dhaifu kiasi hicho. Vijana huwa wanasema ukitaka kujua polisi wapo serious subiri wawe wanakutafuta wewe.
"Kwahiyo kama kuna watu walihongwa polisi wangeshajua mapema na kuwakamata. Wangehongwa wawili, watatu labda wangelinda siri, lakini kuhonga nchi nzima na polisi wasijue ni ngumu kuamini.
"Sehemu kubwa ya vijana walioandamana walikua na madai yao ya msingi. Wapo waliokua wanapinga vitendo vya utekaji. Hawa ni watu waliopoteza ndugu zao, watoto wao au wazazi wao na hawajaona hatua zikichukuliwa kupata haki. Kwa mfano ndugu wa mzee Kibao walioshuhudia baba yao akishushwa kwenye basi na kwenda kuuawa kikatili, hivi wanahitaji kulipwa ili waandamane? Ndugu wa Soka, Mdude, Polepole, Ben Sanane na wengine je?
"Pili, vijana wamedai Tume huru ya uchaguzi na Katiba mpya kwa muda mrefu. Wanataka sauti zao zisikike kwenye sanduku la kura. Lakini wameshuhudia wasimamizi wakitiki kura vituoni na kuziweka kwenye masanduku. Yani msimamizi mmoja anatiki ballot paper 20 anazishindilia kwenye sanduku. Hivi wafuasi wa vyama vilivyoshiriki uchaguzi wakiona hivyo watasubiri kulipwa ili waandamane?
"Mtaani kuna mamilioni ya vijana waliohitimu ngazi mbalimbali za elimu lakini hawana ajira. Wachache walioamua kujiajiri wamekutana na vikwazo vingi vya kimfumo. Leo si ajabu kumkuta graduate anatembeza karanga barabarani na bado mgambo wa jiji watambugudhi na kumwaga karanga zake. Inauma sana. Kijana kama huyu hatasubiri kulipwa ili kuingia barabarani.
"Kesi za kusingiziwa, Tuhuma za ufisadi serikalini, kuminywa kwa uhuru wa maoni, Nepotism ni miongoni mwa mambo yaliyofanya vijana kuingia barabarani ili kupaza sauti zao baada ya kuona wamelalamika kwa muda mrefu bila kusikilizwa. Siamini kama walillipwa.!"
Uko na la kusema tofauti na point za Malisa?
Tumekuta utaratibu na tumeufuata, kuna kukengeuka kwa kulindana!
Kuna vitu haviko sawa, hadi wananch wanaongea na kuchukua hatua hizi kuna mahali hapapo sawa!
Kurudi kwenye uwanja wa mapambano ya kisiasa ilikuwa ni best option!Maamuzi ya kudeal na watu kama Ng'ombe yametufikisha hapa leo!
Kuelimisha vijana wengi kwenye shule za kata mlitegemea business as usual?
Mmeshindwa kwa makosa yenu wenyewe na kujisahau!....changa karata vizuri, otherwise ni matatizo juu ya mengine mnaongeza!...
Na hii ni nchi sio kilabu au kampani, bila maslahi ya watu 60m+ hamuwezi tena!