Malkia wa movie za ngumi Cynthia Rothrock atua nchini Tanzania kula bata

Na kuna kitambaa cha tv pembeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
duuuh ,mbona kama hazeeki, yuko vile vile.
 
namkumbuka sana kwenye movie ya yule bondia mtoboa macho.

yani yule bondia na ubabe wake wote, kwenye mapenz alikuwa anainua mikono juu.
 
Enzi hizo tunamjua kama 'Sinsia' Hehhe kumbe ndo Cynthia.. Alikua ni balaaa
 
Dah maisha yalikua mazuri sana miaka hiyo. sasahivi chadema wameharibu kila kitu.
Hahah,lkn huku wana cynthia wao anaitwa wema sepetu.

In white-collar crime, there are ink stains instead of bloodstains.
 

Arusha. Msanii wa filamu maarufu duniani na raia wa Marekani, Cynthia Rothrock, maarufu Lady Dragon, ametua kutalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Cynthia aliyewahi kushinda tuzo tano za filamu duniani kupitia filamu zake za mapigano, amefikia katika hoteli ya Grumeti Serengeti inayomilikiwa na bilionea wa Marekani, Paul Tudor.

Msanii huyo ambaye ameigiza zaidi ya filamu 31, miongoni wa zilizompa umaarufu ni Lady Dragon Xtreme Fighter na Deadliest Art.

Tangu atue nchini juzi Agosti 26, picha zake zimesambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii duniani.

Hata hivyo, kama ilivyokuwa kwa mchezaji maarufu wa Uingereza, David Backham, safari ya Cynthia ni ya mapumziko binafsi.

Akizungumzia ujio wa msanii huyo mwenye mkanda mweusi katika mchezo wa karate, Meneja Uhusiano wa Tanapa, Pascal Shelutete, amesema umetokana na kazi kubwa ya Serikali, Tanapa na wadau wengine kuitangaza Serengeti.

Shelutete amesema wasanii wengine wengi wakubwa duniani wanatarajiwa kuingia nchini, kutalii kama ambavyo imetokea mwaka huu.

“Mwaka huu umekuwa mzuri katika utalii nchini, tumepata watalii wengi maarufu duniani, wakiwemo wachezaji mpira, wasanii wa filamu na viongozi wa kisiasa,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 
Wale kina Heche na wenzao waliosema VAT inafukuza watalii, je bado kauli ni Ile ile
 
hatari sana umenikumbusha Cynthia Khana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…