TANZIA Malkia wa Uingereza, Elizabeth II afariki dunia akiwa na miaka 96

Pole kwa raia wote wa "UK",Ufalme ulifanikiwa kujenga himaya yenye nguvu sana kwa Machozi,Jasho na Damu...Ni fahari kwa raia wake...lakini pia haiondoi historia mbaya,chungu,katili ya himaya yao kila ilipoacha/kanyaga nyayo zake(Asia,Amerika, & AFRICA nk)
 
Kweli kabisa.

Kwa Afrika ni Libya pekee walikuwa wana hizo fursa.

Wakati nikisoma huko nje miaka ya zamani wanafunzi wenzetu wa Libya wengine walikuwa wakikodisha nyumba nzima peke yake na aishi kama raia wa hiyo nchi.

Ghaddafi alikuwa aliwatunza sana raia wake.

Saudi Arabia bado wafanya hivyo na vijana wao wakiwa nje ndo utafahamu kuwa kule kwao wao hufuata tu sharia kwa uoga kwani hadi mabinti zao wakiwa Ulaya na Marekani huondoa "hijab" na hata kupiga kilauli kufaidi matunda ya ujana.
Safi kabisa mkuu . Yaelekea hawana Uhuru mkuu
 
Wakuu kuna watu bado waulizauliza hapo kuhusu utaratibu wa msiba na hatimae maziko ya Malkia Elizabeth wa pili, ntaeleza kwa ufupi kidogo.

Mwili wake watarajiwa kupelekwa London siku ya jumanne na utalala Bukhingham Palace. Kisha maandalizi yataanza kwa kuupeleka pale Westminster Palace ambako utalala sehemu yenye ukumbi mkubwa wa Westminster Hall.

Hapo Westmenster Hall ndipo watu watapata fursa ya kuuaga mwili na kutoa heshima za mwisho na mwili utaendelea kulala hapo ukisubiri viongozi wa mataifa mbalimbali ambao wataanza kuwasili Ijumaa tarehe 16.

Shughuli ya maziko rasmi ni pale Westminster Abbey na hio itatangazwa na runinga zote kama ilivyokuwa kwa Diana.

Baada ya shughuli zote za maziko kukamilika Jumatatu tarehe 19, mwili wa Malkia wa Uingereza Elizabeth wa pili utapelekwa sehemu iitwayo St George Chapel iliyopo sehemu iitwayo Windsor ambayo ni kama lisaa hivi kutoka London.

Hapo ndipo yalipo makaburi ya kifalme na amezikwa baba yake Elizabeth George wa VI paitwa King George Memorial Chapel na makaburi mengine yote ya ukoo wao yapo hapo.

Phillip mume wake Elizabeth yupo hapo akimsubiri mkewe na watawekwa pamoja.

Hii sehemu ilijengwa kati ya mwaka 1425 na 1528 na makaburi yote yapo chini sehemu iitwayo "Vault" huku juu yake pakiwa na kanisa liitwalo St George Chapel ambalo Mfalme Charles wa tatu na Malkia Koni Camilla walibariki ndoa yao na pia mwanamfalme Harry alioana na mkewe Meghan.

Kuna watu wameuliza kuhusu urithi wa kiti cha ufalme na ni nani anastahiki kufuata.

Mfalme Charles wa tatu ndie alikuwa mrithi wa kwanza wa kiti hicho na wanofuata ni William na watoto wake, Yaani George, Charlote na Louis.

William kwa sasa ndie mrithi wa kwanza baada ya Charles na mkewe Catherine atakuwa Malkia Catherine.

Kisha afuatia Harry ambae ni wa tano katika orodha ya warithi na watoto wake na baada ya hapo wafuatia wengine ambao ni baba zao wadogo William na Harry ambao ni Andrew na watoto wake, Edward na watoto wake

Hivyo Mfalme mtarajiwa baada ya Mfalme Charels wa tatu ni William ambae kwa sasa ana umri wa miaka 40.
Okay
Kote nimeelewa!
Lkn kwann after Charles atafuata mwanae William na sio wadogo zake kina Anne, Andrew...?
Na kwann baada ya William wanafuata wanawe ndipo Harry? Kwanini sio Harry kwanza ndipo wafuate watt ambao ni wajukuu wa Elizabeth?
 
Huo ndo utaratibu wa urithi ulivyo, wenyewe waita "heir to the throne" au "first -in-line to the throne".

Yaani yule wa kwanza akiwa mwanamme basi atakuwa Mfalme na akiwa mwanamke atakuwa Malkia.

Baba yake Elizabeth alipokufa hakuwepo mtoto wa kwanza wa kiume hivyo Elizabeth akawa ndie mrithi.

Mtoto wake wa kwanza wa Elizabeth ni mwanamme ambae ni Charles anarithi na afuatia mtoto wa kwanza wa Charles ambae pia ni mwanamme William na kisha mtoto wa kwanza wa William ambae ni George.

Mtoto wa kwanza wa Elizabeth angekuwa ni mwanamke basi huyo ndie angekuwa Malkia.

Hivyo Charles ni mfalme na William ndie sasa aitwa "Heir to the throne" yaani ni mrithi wa kwanza na wakati wowote aweza kuwa Mfalme na mtoto wa William yaani George ndie sasa aitwa "second Heir to the throne".

Hawa William na George ndo wapo mafunzoni kuja kuwa wafalme wa baadae wa Uingereza. Charlote na Louis ambao ni wadogo zake George, wote ni warithi wa baba yao ingawa watangojea baba yao afe na George nae apite.

Sasa utauliza vipi hao wengine?

Jibu ni kwamba wote hao wapo kwenye mstari yaani "line to the throne na pia heir to the throne lakini ni jambo ambalo halitakuja kutokea Harry awe mfalme au watoto wake.

Hivyohivyo kwa Andrew na Edward ambao ni wadogo zake Charles wao wapeta tu ila pamoja na watoto wao wote wapo kwenye ule utaratibu wa kurithi ingawa ni ndoto kwao.

Jambo jingine la kuelewa ni kwamba hawa majamaa wana sheria ya urithi wa kiti cha enzi cha ufalme na sheria hii yasema kwamba, wale warithi sita wa mwanzo wa kiti hicho wakitaka kuoa ni lazima Ufalme uidhinishe jambo hilo na ukioa bila idhini ya ufalme basi weye na mke wako na watoto wote mwaondolewa kwenye mstari wa urithi lakini ndoa yenu yabakia kuwa halali kisheria.

Sasa hapo kuna mambo mawili makubwa yametokea kwenye familia hiyo hivyo, nakupa kitendawili utafute ni mambo yepi hayo? maana hayo huenda yameathiri au kuathiriwa na sheria hiyo.

Nadhani utaelewa.
 
Charles hakuwa na haki Mama kambeba ingawa alikasirika na akasusa kushiriki ndoa kwa sababu ya dini

Wanajua yajayo
Screenshot_20220919-111036_One%20UI%20Home.jpg
 
Charles hakuwa na haki Mama kambeba ingawa alikasirika na akasusa kushiriki ndoa kwa sababu ya dini

Wanajua yajayo View attachment 2366365
Ni kweli, khasa kulingana na sheria yao inavyosema.

Nafikiri reasoning ya bibi ni kwamba William aendelee kupaliliwa na Charles akae kwa muda.

Lakini wadogo zake Charles khasa Andrew amekuwa ni sauti kuu ya kukataa Charles asiwe mfalme.

Yasemwa Charles aharakisha sana sasa hivi afanyiwe sherehe ya kumrasimisha ambayo itagharimu kiasi kikubwa cha fedha na waizungumzia mwakani mwezi Juni.
 
Hii lugha gani umetumia?
 
Kweli kabisa mkuu
Charles anataka atawazwe haraka ila nafikiri coronation itakuwa hata zaidi ya mwaka

Na huenda asikalie kiti mda mrefu kwani William alianza kufundishwa tabia za kiutawala tangu mdogo sana na Harrry hakuna aliekuwa anamjali sana ndio maana hata night club alikuwa anaenda na hata bangi kavuta

Hata wazawa baadhi hawamtaki mzee na sasa wameanza kusema Camilla hawezi kufuata Mila na mienendo ya Malkia
Malkia alikuwa na wafanyakazi aliewachagua mwenyewe kutoka Aristocrats families na wamemtumikia Malkia kuanzia 1953 na sasa wengine wana miaka 80 imebidi wote wastaafu kwa sababu Queen kafa na hawakuwa wanalipwa mshahara daaa

Sasa Camilla hata secretary wake hajulikani anaenda kivyake tu na wazungu hawataki haya
Nafikiri mke wa Will atafuata nyayo za Malikia
 
Aisee siku zote hizo walikua wanaishije bila kulipwa au huduma zote zilitoka kwa malkia.
Nakufuatilia sanaa najua unajua mengi ukipata wasaa tujuze kwa wingi.
 
Mkuu hawa wanaitwa Ladies in Waiting na kazi yao ni kumuandalia nguo gani atavaa na maandalizi ya chakula na pia appointment zake zote

Hawa wote walikuwepo miaka yote ya utawala wa ufalme na wengine kama wawili walifariki baada ya Prince Philip kufariki wakiwa na umri wa miaka 90

Wote wanatoka katika familia kubwa za karibu na ufalme na wengine walicheza na malikia pia
Wana hela kwa vyeo vyao pia ila mshahara kwa kumtumikia Malkia hawalipwi kwani ni wito na heshima tu
 
Thank you ....nilisoma kama complain flani nmeelewa (lengo ni kudumisha undgu na urafiki)

Kwa nini charles amebebwa na mama yake kua hapo alipo ilhali n mrithi sahihi?
 
Pamoja sana mkuu

Charles alikuwa ana date na Dada yake Diana kabla hawajajuana na Di mwaka 1977
Di alikuwa na miaka 16 wakati huo hivyo hata kiumri walipishana kama miaka 12 na Charles

Dada yake Di hawakuendelea na Charles kwani mapenzi hayakuwa ya moto na kusema kuwa hawezi kuolewa na Charles hata kama ni mfagiaji au Mfalme

Ndipo walipokutana tena Di na Charles kwenye mazishi ya Jamaa yake wa karibu na Charles alieuwawa na Di akamwambia you must be a very sad person kutembea nyuma ya jeneza peke yako bila demu
Charles akamrukia na kumbusu di na kuanza kumfuata nyuma nyuma kila aendapo kama mbwa mdogo ( maneno ya Di mwenyewe)

Di aliwaambia rafiki zake kuwa atakuja kuolewa na Charles maana ni mtu pekee ambae hawezi kunipa Talaka

Ila tatizo likaja alipokuwa na Camilla ambae nae alikuwa wa kukosana na mshikaji wake Andrew Parker Bowles Mara waachane mara warudiane na huku Charles akila

Royal family hawakupenda Camilla aingie kwenye familia na hapo wakamuozesha Charles huyo binti mrembo Di

Ila kimaadili na Sheria zao Charles kumuoa mwanamke alieachika na pia kuachana na Diana ambapo hairuhusiwi na isitoshe ndio Mfalme ajaye

Na Malkia alikasirika na hakuhudhuria kwenye harusi ya Charles na Camilla

Ila Charles anajua hilo na huenda akamuachia mwanae Ufalme soon
 
Thanks sanaa sasa nmeelewa na vip kuhusu harry na meghan ndio watakaa pembeni au wataendelea kua wana wafalme.

Najua nakusumbua sanaa ila kwa wakati wako naomba unijibu.
 
Pamoja na ukweli kuwa Harry aliachia cheo cha HRH au His Royal Highness lakini bado yupo kwenye line ya utawala kama mmoja wa familia

Meghan atakuwa Queen Consort kama Harry atakuwa Mfalme kwa kuwa mke wake sio damu ya familia hii
 
Naomba unifahamishe kidogo, yawezekana hii stori ya Harry na Meghan imenipita.

Nini sababu ya Harry na Meghan kuwa nje ya Royal Grounds?
 
Kweli kabisa.

Kwa Afrika ni Libya pekee walikuwa wana hizo fursa.

Wakati nikisoma huko nje miaka ya zamani wanafunzi wenzetu wa Libya wengine walikuwa wakikodisha nyumba nzima peke yake na aishi kama raia wa hiyo nchi.

Ghaddafi alikuwa aliwatunza sana raia wake.

Saudi Arabia bado wafanya hivyo na vijana wao wakiwa nje ndo utafahamu kuwa kule kwao wao hufuata tu sharia kwa uoga kwani hadi mabinti zao wakiwa Ulaya na Marekani huondoa "hijab" na hata kupiga kilauli kufaidi matunda ya ujana.
Na kitimoto wanafakamia balaa
 
Back
Top Bottom