KERO Malori yanayochukua vifusi Mbutu- Kigamboni hayafuati sheria za usalama barabarani

KERO Malori yanayochukua vifusi Mbutu- Kigamboni hayafuati sheria za usalama barabarani

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Eneo Mbutu limekuwa sehemu kuu ya kuchimbwa vifusi kwa ajili ya ujenzi mbalimbali.

Hatari kuu kwa watumiaji wa barabara ni haya malori kujaza vifusi kupita kiasi kinachotakiwa na hakuna hatua inayochukuliwa na mamlaka husika.

Moja ya madhara ambayo yamekuwa yakitokea ni kumwagika kwa vifusi barabarani hali ambayo inahatarisha usalama kwa watumiaji wengine wa barabara.

Askari wa usalama barabarani tunawaona wapo ila hawachukui hatua za kukomesha hii hali.

Ukichanganya na ubovu wa barabara kwa sasa tunaomba mamlaka husika ikiwemo TARURA, TANROAD na vikosi vya usalama barabarani kiuchukua hatua haraka kabla madhara zaidi hayajatokea

20250109_120728.jpg

20250109_120544.jpg
 
Keep distance driving mna someaga vichochoroni
 
Back
Top Bottom