Huwezi kujua unachokizungumza halafu ukawa na baridi au aibu au kigugumizi kukizungumza. Unatia mashaka.
Kuna mwaka tulifukuzwa kwa muda kama wa miezi 6/7 wengi tukajua ndio imeisha safari ya elimu ya juu.. kwa kosa la kugoma, kipindi cha Hayati Mzee Mkapa.
Waliosalia walikuwa first year, lengo la serikali lilikuwa ni kuzalisha kizazi kitakachoogopa mamlaka, si kuheshimu, ili vyuo vipoe na vitawalike.
Imefanya kazi kwa zaidi ya miaka 12 hakujawa na migomo katika vyuo vikuu, hii haimaanishi Hali ni nzuri sana, ila serikali imefanikiwa kutengeneza kizazi Cha wasomi wenye inbuilt hofu ya mamlaka na wenye mamlaka.
Tatizo ni kuwa na wasomi wasiojiamini, wavivu wa kwenda extra mile.. as a result persistence na that urge to defy the status quo for the pursuit of knowledge and excellence inakufa among wasomi, wengi sio wanaishia kuheshimu mamlaka tuu, ila wanaishia kuheshimu notice za mwalimu tuu.. now that's deadly