Kichwa kama cha MSALANI,SIMIYU YETU,LUSUNGO,LUKOSI NA SAMPLE Zingine kama hizo ndiyo unategemea waelewe kweli,Yaani magamba kichwani yamejaa madudu.
Nimempenda sana Humphrey Polepole.Katika mkusanyiko ule nampa maksi nyingi sana.Kwanza anaelewa vizuri sana anachozungumza.Na kwa kweli kawaacha mabali sana kwa kufikiri.Anatumia hoja kujibu hoja.
Mtazame mtu kama,
Monday Likwepa: Hana hoja zaidi ya kumtukana Warioba.Anamjadili Warioba badala ya maoni ya tume.
Godwin Kunambi:Huyu naye ni mwanasheria wa CCM lakini hana kitu kichwani.Hana hoja ya msingi aliyojadili badala ya kutoa povu.
Simon Simalenga:Mwigizaji huyu aliyepewa cheo Clouds Media naye hana uelewa wa masuala ya kijamii.Eti takwimu zile ni chache sana, watanzania hawakuulizwa.Data hizo ni zao kina Warioba.Ina sikitisha sana wachangiaji wa jana waliharibu sana. Simalenga alisema eti watanganyika hawapo kwa hiyo hakuna aliyeulizwa swali hilo.Lakini upande wa pili anasema Wazanzibari na Watanzania bara hawakusema wanataka serikali tatu.Hajui kuwa kafanya tautology.Huwezi kuwa na watanzania halafu humo ndani umewatoa wazanzibari.
Ukweli halisi ni kuwa wenye maslahi tu na mfumo uliopo wanashabika serikali mbili.WEngine walisema eti wazanzibari hawataki serikali tatu.Ni sawa wakisema hivyo kwani wao wana serikali yao.Sisi ndio tunaopaswa kuidai serikali yetu.Tulikubali vipi kuifuta na kutumia jina la Tanzania?Maoni yao ya jana yalikuwa hovyo kabisa na wengi pale waliitwa kichama zaidi. Mchungaji Alphonce naye ni mnafiki sana.Lazima ana agenda ya siri. Kweli haoni matatizo ya Muungano huu?Viongozi wa dini wenye unafiki lazima walaaniwe.
Deus Kibamba nilimwona kama mtu mwenye chuki na tume ya Warioba.Kuna jambo limejificha.Anasema tume haikutembea kila kata na kila kijiji.Hivi kazi hii angepewa yeye angepita kote huko? Tume ngapi zimewahi kuzunguka kila kijiji cha nchi hii?Hata tume ya Jaji Nyalali haikupita kila kijiji.Tujiulize mbona tuna Rais wa nchi lakini hadi anamaliza miaka 10 madarakani hatembelei kila kata ya wilaya?Sembuse tume iliyokuwa inakimbizana na muda?
Mwingine naye akasema eti wao walipewa kazi ya kukusanya maoni tu na kuyapeleka kwa Rais na tume ikafanya kazi ya kuchambua.Hivi ni kweli kuwa Tume ingeleta kila maoni kama yalivyo huyu Kikwete angeweza kweli kuyapitia yote?Ikiwa miswaada tu mingine anasaini bila kuisoma kikamilifu.Kitabu cha biblia pia kimesema na mchungaji Alphonce anajua kuwa si kila alilofanya Yesu limeandikwa kwenye biblia ingekuwa hivyo ulimwengu usingetosha kwa wingi wa vitabu.Tujadili hoja na si kumtukana Warioba.