Hapana, hapa kuna kamchezo kachafu kametokea, yawezekana tumechezewa, au ni changa la macho hili. Huyu Mrema wa sasa siye yule Augustino Lyatonga maarufu mzee wa Kilalacha, huyu wa sasa siye, ndio nalazimika kuamini kuwa "wachina" pengine wamefanya vitu vyao, au pengine ni zile tabiri zilizotolewa mwanzoni mwa mwaka huu na mbashiri yule wa pale magomeni, labda, lakini mwenzenu Mrema huyu wa sasa simwelewi, sijui amekutwa na nini jamani.
Hivi mwakumbuka kauli zake za toka 1995? hasa wakti akijiuzulu uwaziri wa Mambo ya ndani, ubunge na hatimaye kuhama chama na kwenda NCCR kabla ya kwenda uko aliko sasaivi?
Wana JF najua hapa ndo kisima cha yote haya, naomba mwenye kumbukumbu ya kauli za mzee wa Kilalacha tukumbushane jamani, je kweli huyu ndiye yule yule au pengine ni miye tu ndo namwona tofauti?