Asante umekubali alikuwa mchapakazi na afadhali unasema angekuwa dictator, dictator wa aina ya Mrema ungekuwa mazuri na kwa mafanikio kwa taifa( haya maoni yangu) nchi zetu hizi ili ziendelee zinahitaji dictator piga ua!, dictactors can be valuable to any country kama tu wanafanya mambo yaende kwa manufaa ya umma! that is how china it is today!
Nyerere na Sokoine walifeli kwenye hilo eneo
Sasa hapa Ben kwa mimi ndio huwa nauliza tatizo ni Mrema au sisi wananchi? Mrema alikuja kwa wananchi tukamkataa , kaenda huko na huko tumemkataa!, hii ni same story kwa wapinzani wote tusipowakubali watarudi nyuma! kurudi nyuma huko ni aidha akae kimya, au arudi CCM, ebu jiulize leo hii let say Slaa akasema hana hela ya kula kabisa, are we ready kuchanga fedha yeye na familia yake aishi?? it was the same kwa Lwamwai kasaga lami wakati kaporwa vyeti vyake na CCM, alikuwa hane mbele wala nyuma, just imagine froe being lecturer UDSM mpaka kuishia kuomba hela ya nauli! mtu ana familia yake!!!
watu wa aina ye Mrema watajitokeza sana, pale wanapoona future yao haiko clear, na wananchi hawana mpango nao, then nife kwa sababu mpinzani?
Tukubali tu vyama vya siasa vina udhaifu mwingi sana, lakini na sisi wananchi tunachangia mno kurudisha wapinzani nyuma!
Mrema atabaki kama mpinzani pekee bara ambaye rekodi yake haijaweza kuvunjwa kwa miaka 16! na inavyoonekana inaweza isifikiwe tena kama opposition wasipojipanga. Mrema is still above all kwa alichofanya, tena kumbuka alivuta watu kipindi Nyerere yuko hai!
Mrema anabaki mwana CCM pekee asiye mnafiki kujifanya unapigania ufisadi ukiwa ndani ya CCM! aliondoka bila kuangalia nyuma, na alitikisa nchi.
Mrema anabakia mtu pekee ambaye hata rekodi yake ya utendaji ndani ya wizara aliyoongoza hakuna aliyeweza kuvaa viatu vyake!
Na anabakia kuwa mtu pekee ambaye anakuwa muwazi wa kile anachokiamini hata kama hatukipendi, vinamfanya kuwa yeye! LOL!
Leo hii Mrema is still politician lakini anafaa zaidi kuwa CCM na kupiga kampeni akiwa CCM, na si vinginevyo, mafanikio na rekodi zake haziusaidii upinzani kwa sasa isipokuwa an haribu, tena vibaya mno