Bwana A L Mrema ana haki kabisa kumburuza mahakamani Mheshimiwa S Sitta kama anaona amekashifiwa.Ikumbukwe Bwana Mrema si mtu wa kwanza kukimbilia mahakamani kwa kukashifiwa wako kina Mheshimiwa Rostam Azziz,Reginald Mengi,Yusuph Manji na wengineo kibao kinachonishangaza wote hawakuitwa machizi,wameathirika au punguani kwa kwenda mahakamani kutafuta haki.
Mheshimiwa S Sitta anaweza kujikuta katika matatizo ambayo kwa hakika angeweza kuyakwepa,kutoa kauli kwamba fulani kafilisika kisiasa nadhani si kosa lakini unapokwenda mbali zaidi kusema fulani kaishiwa hana fedha kwa maoni yangu nadhani hiyo ni kashfa unless aweze kuithibitishia mahakama bila shaka yoyote.