Mama afariki, mwanaye anusurika baada ya gari kutumbukia baharini

Mama afariki, mwanaye anusurika baada ya gari kutumbukia baharini

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Winnie Achieng (33) amefariki dunia baada ya gari alilokuwa akiendesha kutumbukia katika bahari ya Hindi mjini Mombasa, Kenya huku mwanaye wa miaka 12 akiogelea hadi ufukweni.

Taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi inaeleza kuwa Winnie alifariki wakati akipatiwa matibabu hospitali muda mfupi baada ya kuokolewa.

Inaeleza kuwa alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Vitz akitokea eneo la Changamwe kwenda mjini Mombasa akiwa na mwanaye wa kiume mwenye umri wa miaka 12 ambaye alifanikiwa kuogelea na kutoka ndani ya maji.

“Mtoto alifanikiwa kuogelea kabla maji hayajamzidi nguvu lakini mama yake alishindwa kutoka ndani ya gari kutokana na mkanda kumbana hadi pale alipokuja kuokolewa na wasamaria wema huku akiwa ameshakunywa maji mengi.”

“Baada ya kufanikiwa kujiokoa kutoka kwenye maji mtoto alikuwa na majeraha kadhaa
katika mwili wake ambayo alitibiwa hospitalini kabla kuondoka na baba yake kwenda nyumbani,” inaeleza taarifa hiyo.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Omar Chigamba, amesema kuwa aliona gari hilo likiendeshwa kwa kasi kabla ya kuingia baharini na alikimbia kwenda kuwaokoa waliokuwa kwenye gari lakini alimkuta mama huyo akiwa katika hali mbaya.


12.JPG


Chanzo: Mwananchi
 
Poleni ndugu jamaa na marafiki.

Kenya hii ajali ya pili kwa mama kutumbukia babarini.
 
Apumzike salama.
Tuchukue tahadhari,mwendokasi ni hatari .
 
R I P
Mama Mtu

Mikanda imekua changamoto Kwenye kujiokoa
Nakumbula ile ajali ya roli lililowaka moto Morogoro na kuuwa watu.

Dereva wa lile roli kabla ya moto kulipuka alikua hajafa,alipiga kelele,jamaa mmoja akaenda kujaribu jumuokoa kwenye kibini ya roli,ila alishindwa kwasababu ya mkanda(seat belt).

uyo muokoaji aliona hatari ya uwezekano wa ilo roli kulipuka akaamua kuacha harakati za kumuokoa akasepa,baada ya kufika umbali wa mita kumi chuma ikaitika moto ukawaka.
 
Apumzike kwa amani.. marehemu ana age gap nzuri sana na mwanae.. mama 33 mtoto 12yrs...maana yake alizaa akiwa 21
 
Hizi picha ndio kigogoo aliziedit zikawa kama na giza giza flani, akasema hizo ni maiti za watu waliouawa Zanzibar kipindi cha uchaguzi na kutupwa baharini na wanajeshi.
 
Wawe wanakua na mkasi kwenye gari
Kipi rahisi:

kutafuta mkasi ulipo, ku reach kuuchukua, na kukata mkanda katikati ya moshi, moto, maji au giza na gari iko miguu juu

Au

kubonyeza kifundo chekundu cha ku release mkanda ?
 
Back
Top Bottom