Keyboard_Warrior
JF-Expert Member
- Oct 10, 2015
- 6,381
- 11,296
Habari ndugu zangu?
Issue iko hivi, dogo yupo kidato cha nne, anasoma shule ya sekondari IGANZO, ipo mkoa wa Mbeya.
Mwezi wa sita mwaka huu walifunga shule, lakini kwakuwa yupo kidato cha nne, walimu waliwaambia wanafunzi kuwa kidato cha nne hawatokuwa na likizo ya mwezi wa sita, wanatakiwa kuendelea na masomo ili kujiandaa na mtihani wa taifa wa kidato cha nne.
Ila walipewa sharti kuwa kila mwanafunzi wa kidato cha nne atatakiwa kulipia shilingi elfu kumi (10000) ili aendelee na masomo, hii sio hiyari ni lazima.
Dogo amerudi nyumbani, lakini Bi mkubwa wake hayupo, ni single madha, ameenda mkoa mwingine kwenye harakati zake za utafutaji.
Dogo amempigia simu Bi mkubwa wake kumpa taarifa kuhusu habari ya kuendelea na masomo kipindi cha likizo, Bi mkubwa wake anamjibu dogo kuwa hana hiyo pesa, mambo yake yapo vibaya. Kwahiyo dogo inabidi akae tu nyumbani mpaka likizo itakapoisha.
Likizo imeisha, dogo anaenda shule walimu wanamzuia kuendelea na masomo. Wanamuambia arudi nyumbani, akamuite mzazi, pia aende na shilingi elfu kumi (10000) pamoja na mfuko mmoja wa cement.
Muda huo Bi mkubwa bado hajarudi safari aliyoenda, dogo anawaelekeza waalimu kuwa mzazi wake amesafiri hayupo, walimu wanakataa kumuelewa.
Dogo anaamua kukaa nyumbani kumsubiri Bi mkubwa arudi.
Juzi Bi mkubwa amerudi, jana ameenda na dogo shule.
Baada ya kufika shule, walimu wanamuambia Bi mkubwa kuwa inabidi asaini barua inayoelekeza kukubali mtoto wake kuacha shule, kwasababu mtoto wake ni mtoro. Bi mkubwa anawaelekeza kuwa hali yake ya kifedha ilikuwa mbaya, alikuwa anauguza pia, lakini walimu wanagoma kabisa kumuelewa.
Walimu wanamuambia kama amegoma kusaini barua ya mtoto kuacha shule, basi amchukue mtoto wake arudi naye nyumbani, lakini shuleni hawataki kumuona, pia walimu wanasema hawataki SIFURI shuleni kwao, dogo atawaletea SIFURI shuleni.
Mwisho waalimu wanamuambia Bi mkubwa kuwa akitaka aende hata wizara ya elimu, lakini wao hawana msaada mwingine kwake.
Dogo anaitwa KEVIN FREDRICK MSOMBA