Mama akataa zawadi ya gari kutoka kwa mwanawe, adai 'hili ni Jeneza', amshutumu kwa Freemason

Mama akataa zawadi ya gari kutoka kwa mwanawe, adai 'hili ni Jeneza', amshutumu kwa Freemason

Mwanamke mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni Mama wa msanii wa muziki Bongo, Hamisi 'Tajiri Chui' Mwelemi amekataa gari jipya alilopewa na mwanawe huyo, akidai kuwa zawadi hiyo inahusiana na shughuli za Freemason.
View attachment 3190836
Akiwa na msimamo mkali, mama huyo alidai gari hilo "ni jeneza" na kuonya kuwa hataki kushiriki lolote linalohusiana na imani au makundi yasiyoeleweka.
View attachment 3190838
View attachment 3190842
Ila hili gari sio jipya ni mtumba na thamani yake haizidi 20M
 
Yale matapeli yanayodai kuunganisha watu na ufreemason yameharibu akili za watu. Zile picha za maburunguti ya hela, majumba na magari zimewaaminisha watu kuwa huo utajiri wanatoa wao. Ikitokea kijana kapambana wee akapata gari au jumba watasema tayari amejiunga freemason, ataanza kuogopwa na ndugu zake kwa dhana kwamba watatolewa kafara. Kumbe hakuna kitu wala freemason hawahusiki, huko ni kutokujua dhana ya freemason in and out
sasa huyo jamaa, si ndio michongo yake ya kujifanya freemason then anawapiga watu huko tik tok, anazipa hela media zinapiga promo miyeyusho yake. sijui na mimi nifanye haya maigizo wabongo ni wehu, wanajiunga kwa kulipia ma group yake
 
Huyu sijawahi msikiaa .....huko mjini ni nani??
 
Sasa mama kama anaona mtoto wake Hana vyanzo vya kueleweka vya kupata huo utajiri apokee tu?hapa ndipo wazazi wengi walipofeli kwenye malezi ya vijana wao.
 
Hii nchi kumbe kubwa sana, hv kumbe huyu naye ni msanii?
 
Wale wapuuzi walioanza kuisema vibaya Freemason miaka ya 90's na 2000 mwanzoni wameharibu sana watu
nasikitika kusema wale masheikh uchwara kutoka kenya wameharibu mbongo za watu vibaya sana
 
Back
Top Bottom