The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Katika kuadhimisha Siku ya Watoto Njiti Duniani, Taasisi ya Doris Mollel imemkabidhi nyumba ya makazi Mariam Mwakabungu (26), aliyejitolea kukumbatia Watoto Njiti katika Hospitali ya Rufaa Amana jijini Dar es Salaam, yenye thamani ya Shilingi milioni 45, iliyopo Chanika – Zavara.
Mariam amezawadiwa nyumba hiyo na msamaria mwema (hajataka kutajwa jina), ambayo imejengwa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kwa kushirikiana na wadau wengine waliochangia baadhi ya vitu wakati wa ujenzi wake.
"Napenda kumshukuru mungu, pia natoa shukrani za dhati kwa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, sina kingine cha kuwashuru ni kama vile nimeshtuka ndotoni, pia naomba kuwashukuru Wizara Ya Afya na Hospitali ya Amana, kwani wasingekuwa wao sijui ningekua wapi..." - Alisema Mariam.
Soma pia: Mwanamke anayejitolea kukumbatia Watoto Njiti waliotelekezwa Hospitali ya Amana
Julai 20, 2023 serikali kupitia Wizara ya Afya, ilitoa ajira ya mkataba kwa Mariam, ikiwa ni siku moja tangu Rais Samia Suluhu Hassan kutuma salamu za pongezi zilizoambatana na fedha taslimu.
Chanzo: Azam TV