Mama aliyejitolea kukumbatia watoto njiti akabidhiwa zawadi ya Nyumba, abubujikwa machozi baada ya kufanyiwa suprise

Mama aliyejitolea kukumbatia watoto njiti akabidhiwa zawadi ya Nyumba, abubujikwa machozi baada ya kufanyiwa suprise

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Katika kuadhimisha Siku ya Watoto Njiti Duniani, Taasisi ya Doris Mollel imemkabidhi nyumba ya makazi Mariam Mwakabungu (26), aliyejitolea kukumbatia Watoto Njiti katika Hospitali ya Rufaa Amana jijini Dar es Salaam, yenye thamani ya Shilingi milioni 45, iliyopo Chanika – Zavara.

Mariam amezawadiwa nyumba hiyo na msamaria mwema (hajataka kutajwa jina), ambayo imejengwa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation kwa kushirikiana na wadau wengine waliochangia baadhi ya vitu wakati wa ujenzi wake.

"Napenda kumshukuru mungu, pia natoa shukrani za dhati kwa Taasisi ya Doris Mollel Foundation, sina kingine cha kuwashuru ni kama vile nimeshtuka ndotoni, pia naomba kuwashukuru Wizara Ya Afya na Hospitali ya Amana, kwani wasingekuwa wao sijui ningekua wapi..." - Alisema Mariam.

Screenshot 2024-11-19 114047.png

Soma pia: Mwanamke anayejitolea kukumbatia Watoto Njiti waliotelekezwa Hospitali ya Amana

Julai 20, 2023 serikali kupitia Wizara ya Afya, ilitoa ajira ya mkataba kwa Mariam, ikiwa ni siku moja tangu Rais Samia Suluhu Hassan kutuma salamu za pongezi zilizoambatana na fedha taslimu.

Screenshot 2024-11-19 114108.png
Screenshot 2024-11-19 113228.png

Chanzo: Azam TV
 
Dorris hapewi maua anayostahili Ila katika NGO's za watu waliotokea kwenye platforms za muziki, filamu au Miss Tanzania kama yeye, anafanya kazi na inaonekana
 
Safi Sana.....!
Hongera Sana Kwa Hiyo Bidada.
 
Kwa hakika anastahili, hicho alichopata ni kidogo sana kwa yale mapenzi makubwa aliyoonesha, hakika mola atamlipa sawa na hiki akifanyacho.

Pongezi pia kwa waliojitolea hiyo nyumba.
 
Safi sana aiseee watu wanaofanya kazi kwa
Moyo mmoja watunukiwe aisee mi wale watoto nawaogopa nyie
 
Back
Top Bottom