Mama anamtetea mke wangu pamoja na kunisaliti

Mengi umeyasoma,mengi umeyasikia,mengi umeelezwa.

Ziba masikio anza moja, Lea watoto wako ukiwa na mkeo, suala la kushiriki tendo la ndoa na mkeo ni maamuzi yako kama umeamua kutoshiriki naye pia sawa.

Lkn Fanya yote angalia afya ya watoto wako,kila kitu tizama watoto wako, wazazi wako wamekuletea ujumbe mzito saana fikiria Mara mbilimbili.

Ni sababu zipi zinazokufanya wewe mpaka Leo unaamini baba yako ndiye baba yako na si MTU mwingine.

Halafu hivi unapata uchungu gani? Kuchapiwa mke ambaye umezaa naye watoto wawili mkwara ulioupiga ulitosha kabisa naye hatua aliochukua kwenda kwa wazazi wako ni sawa kabisa.

Na hata wazazi wako kumleta mkeo kwako ni sawa kabisa,ila hatua zako ulizochukua ni mbaya saana na nampongeza mkeo kuwa ngangari.

Mrudie mkeo kuna watu wamepitia magumu zaidi ya hayo na wako kwenye ndoa imara saana nakupa kisa cha kweli cha mfanyakazi mwenzangu .

Yeye alipata safari ya kikazi muda mrefu aliporudi alimkuta mkewe mjamzito alimuuliza mimba ya nani? Mwanamke hana la kusema, jamaa akawa analala na panga mchagoni.

Mwisho wa siku mke kwa hofu akajifungua watoto njiti wote wakafariki, jamaa yeye ni Muislam kwa kitendo kile cha mkewe alimwambia ataoa mke wa pili.

Na alifanya hivyo mpaka Leo jamaa ana wake wawili na maisha yanakwenda. Kuchapiwa ni siri ya ndani, INA uma saana kwa wachumba na ndoa changa.

Wakongwe hujaona nini? Hujasikia nni? Kama wewe una wivu kweli mtafute kwa panga yule aliyeonja tunda lako.

Pigania maisha kuwa mchungu kutafuta maendeleo, hakika wanao wanasononeka saana hakikisha yule binti wa kazi anarudi na maisha yanasonga.
 
Nimekupenda point zako.Akizichukua akazitendea kazi atakuwa amewin

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu watu hawasomi vizur na wanajua mioyo ya wanaume na wanawake ni sawa kumbe sio.
Soma hapa Mathayo 19:8 Yesu akawajibu Mose aliwaruhusu kuwaacha wake zenu sababu ya ugumu wa mioyo yenu.

Huyo mwanamke ni mpuuzi sana yani yeye badala ya kuendesha familia analeta mchepuko ndani kabisa tena rafiki wa mume?
God forgive this woman sikushangai mkuu hata ulipoleta mchepuko na kuushughulikia nyumbani japo umekosea sana sababu ya watoto i know umewaharibu hapa.
Sikulaumu sana kitendo alichofanya mkeo kilikufanya kichaa muda mfupi.
Ukiona mwanamke anakushauri msamehe jua nae mle mle.
 
Piga chini huyo mwanamke kwani hakukuonea huruma kwa sababu hizi
1 mshahara wako alikuwa anampongezea mwanaume mwengine babaada ya kwichikwichi
2 nyumba uliyo jenga kujistirisha wewe na familiya yako ilikuwa pango la ngono kwa mkeo ,
Kumbuka hata DANGURO NI NYUMBA ILA SI NYUMBA ZOTE NI DANGURO
3 alipuuzia kiapo cha kanisani
4 kuzaa na mwanamke kilimfanya achipuke kwani alijuwa watoto ndiyo ngao ya hiyo ndoa
5 kutoa msamaha kwa mwanamke msaliti ni sawa na kuhalalisha aendelee kuwa msaliti
6 ukimsamehe utaishi naye ktk ile ile nyumba ? Kama ukiishi naye pale pale basi hakikisha yule mfanya kazi wa ndani akamtafute akae naye pia hata yule aliye kuwa anamgegeda endelea kuwa rafiki yako ukifanikiwa vyote ndo utajuwa nini maana ya kutosamehe au kusamehee
7 tangu 2012 nani alikuwa anamkwichikwichi huyo mkeo ili hali mpaka 2017 hukumkwichi kwichi ?
NGAMIYA NI MVUMIKIVU WA KIU LAKINI AKIONA MAJI ANAYATAMANI
NA KUMBUKA
JASIRI HAACHI ASILI
8. angalia msamaha wako usije ukawa uhalalisho wake wa kuongeza michipuko kwani haba na haba hujaza kibaba
9 alijiuliza kuwa matendo yake ndiyo mapambo yake
PAMBO LA MWANAMKE SIYO UREMBO BALI NI TABIA NA STARA YA KUSITIRI HESHIMA NA UTU WA MME WAKE
Jee wewe umeona pambo lake liko wapi
10 JASHO LAKO SI LAKE ILA WATOTO WAKO NI MATOKEO YA JASHO LAKO WEKA NGUVU KUBWA SANA KWA WATOTO WAKO


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuzaa na mwanamke hakumuhalalishi ajichipushe , mtoto siyo ngao ya kumlinda mwanamke ktk ndoa
Yeye hakulijuwa yanaweza kutokea mabaya

Sent using Jamii Forums mobile app
Piga chini tu
Nimekupenda point zako.Akizichukua akazitendea kazi atakuwa amewin

Sent using Jamii Forums mobile app



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi ipo
 
mkuu fanya fuatayo

1. kiungwana ulitakiwa umkazie kwa kutoshiriki nae na kumrudisha nyumbani lakini bila kumufanyia hivo visa vya kuleta mwanamke nyumbani wala kuwa na demu mtaani kwenu hii ingesaidia kwa baadae kurudiana kwa ajili ya watoto wenu sasa hivi katu usirudiane maana uzeeni utalia na kusaga meno kwani atakuja lipiza vibaya sana au atakutanguliza mbele za haki

2. unachotakiwa kufanya ondoka home muachie nyumba na mali zote zisizohamishika kwa ajili ya watoto wewe sepa na hela kaoe mke wmingine na katu usiende mwambia madhaifu ya huyo mke wako huyo utakae muoa
 
Pole mzee baba, ulikosea kumpokea alipoletwa na wazazi, hapa ndipo ulipopigwa.
Binafsi yalinikuta japo ni tofauti kidogo, wazazi walinijia juu mbaya kuhusu kumrudisha, mama akatishia hadi kuniachia laana nikamwambia we niachie tu hiyo laana mama haina shida, baba akawa mkali nikamwambia bora aniue, naona walikaa wakaona huyu mtu yupo tayari kwa lolote tutampoteza wakaachana na mimi.
 
una wasiwasi kuwa hutaweza kujenga tena nini, zaidi ya miaka kumi upo tu mnagombana hata wewe naye ni tatizo
 
kama ametubu na kujutia kosa lake, huna budi kumsamehe for the sake of your children. Akija mama mwingine anaweza akakuvuruga kuliko huyo.
Acheni kushauri upuuzi jamani et km katubu niliwah kudanganyika ktk jambo hilo kilichonikuta mpk nililazimika kudanganya kuwa nimemeza dawa nyingi za kunitoa uhai mwanamke kaogopa kaondoka....sameh mengine yot siyo usaliti hasa wa mwanamke cz mwanamke akikusaliti kadhamiria kabisa Wala si bahati mbaya!!!
 
Mtoa mada ulifanya maamuzi sahihi kabisa, Yaani mwanamke amekusaliti mpaka akaleta mchepuko kitandani kwako huyo mwanamke Hana akili hata robo, Yaani ukiendelea kukaa hapo utakufa muda sio wako! Kama hataki kuondoka ondoka wewe muachie maisha yake na kama ni nyumba uza mgawane au kama hutaki kuuza muachie yeye na watoto waishi itakuwa unakuja kuwaona watoto tu, Yaani alishindwa kuvumilia MIEZI 3 tu!! Na inaelekea hayo mahusiano na huyo RAFIKI Yako walikuwa nayo kabla maana sio RAHISI mke wa mtu akajiingiza kwenye mahusiano ya haraka kihivyo any way pole sana Kwa yaliyokukuta , kitendo Cha KULETA mwanamke mwingine ndani na wewe kufanya nae mapenzi hapo napo na ww uliongozwa na uswahili
 
huyo ni mshenzi tu.... wewe hukuwa na haja ya kumfanyia visa.... endelea tu na maisha yako ya kawaida usimfukuze wala usihame.... rudi nyumbani nenda kazini fanya kama unaishi na mdogo wako..... ishi kiume...
 
Huu ushauri sio kwa kweli.
Mke Malaya HARUDIWI.

#YNWA
 
Kilichokuwa kina kuweka hapo ni watoto sasa hawapo unafanya nn, ondoka kaanze maisha kwingine
Unabahati kupata mahali watoto wanapapenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…