Mama anamtetea mke wangu pamoja na kunisaliti

Mama anamtetea mke wangu pamoja na kunisaliti

siku hizi wanatumia watoto kama chambo ni huruma

kwa kweli Dunia imevaa chupi ishaacha kuvaa kimin imebaki na chupi

utasikia nikiondoka nitaacha wanangu lkn mtu yuko radhi kuingiza wanawake au wanaume kwenye nyumba ya familia na kulala naye kitanda alalacho mkewe au mumewe hii kwakweli ni PHD ya uzinzi sio bure

Heshimu kitanda cha mwenzako aliyeenda kutoa/kuipokea mahari na kamwe mwanaume au mwanamke mwingine hana haki ya kulala kitanda hicho as far as kiapo chenu cha ndoa hakijatenguliwa hiyo ni laana na haiwezi kukuacha salama
 
MKUU NEXT TIME UKIPATA SAFARI YA NG'AMBO NENDA NA MKEO au MPELEKE KWA WAZAZ WAKO
 
kabisa mkuu
 
Kumbe wewe mtu wa Mkoa na siyo born town ndiyo maana huyo demu amekuzingua ameshakuona wewe mlugaluga, madem wa town tunawezana nayo sisi wa town!
Mkuu umeongea kitu usichokijua. Wazee kule kwetu wakikusikia kama hivi wanakuambia kijana tema mate chini sema "Mungu uniepushie mbali na jambo kama hili".
Hao watu ni vigumu kuwaelewa na wanaume waaminifu ndio wanaumizwa kwa kugongewa. Kifupi hao watu wengi wao wenyewe hawajui wanataka nini toka kwa mwanaume. Akipata hiki ukampatia anatamani kile. Yaani ukiwa na pesa yeye anatka mashine, ukiwa na mashine yeye anataka pesa, ukipiga mashine hasa yeye analalamika anataka mtu asiepiga sana, ukiwa na kibamia anataga dushe kubwa, ukiwa na dushe kubwa anataka kibamia.
 
Kwanza; nakuunga mkono katika principle yako. Hata mimi ntasamehe hata uchawi mara zote, lakini usaliti, hapana kwa kweli.
(Tena kwenye nyumba yako, na rafiki yako. Hapo hapo watoto wanapokaa. Aisee, sishauri msamaha)

Pili; Solution ni wewe kusepa, kama yeye imeshindikana.

Tatu; kuhusu watoto...
I mean, sasa unadhani utafanyaje? Tengeneza tu mipango ya wao kuishi kwa namna nyingine.
Hii kauli ya 'for kids sake' waachie wanaoiweza. Wewe unaonekana huwezi, hivyo usiji-force.

Ni suala la mikakati ya watoto wako na wewe tu! If I were you, I'd consider my wife dead. B'coz ume-share na rafiki yako. Sio mkeo tena. Huyo ni mwanamke tu uliyezaa naye.

Damn, this really got into me!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mnaotoa ushauri kama unatoa ushauri kwa wanandoa toeni ushauri wa kujenga especially kwa situation kama hii na sio wa kubomoa hasa hasa kama watu wana watoto. Kwakweli nimeupenda ushauri wa [HASHTAG]#miss[/HASHTAG] chaga

Ijapokuwa mwisho wa siku mume na mke ndo wenye maamuzi ya mwisho
 
Ni kweli huyu jamaa hawezi kuvumilia eti kisa watoto. Sio kila mtu anaweza, kama angekuwa anaweza hasingeleta mwanamke mwingine ndani kulipiza kisasi.
Jamaa awapeleke sehemu watoto aachane na huyo demu vinginevyo watauwana tu. Huyo king'ang'anizi akishindwa kumbadili msimamo jamaa mwisho atamuuwa jamaa kwa sumu au kwa kukodishia majambazi.
 
MKUU NEXT TIME UKIPATA SAFARI YA NG'AMBO NENDA NA MKEO au MPELEKE KWA WAZAZ WAKO
Kwa hivyo huko kwa wazazi wa mume ndio hatagongwa? Mke wa jamaa flani aliomba kutembelea ukweni na huko huko ugenini ukweni kaenda kugongwa na dogo tu jobless alikuwa anauza duka la mjomba wake. Mumewe alikuwa muajiriwa ambae yupo vizuri tu na alikuwa anampenda na kumuhudumia sana mkewe. Malaya ni malaya tu. Yaani huyo mtu ni ndugu yangu wa karibu sana hii stori sio ya kusikia bali mimi ni kati ya waliotumwa kufanya fumanizi kwa niaba ya ndugu yetu.
 
Wakuu habari zenu,

Mwaka 2012 nilienda kozi nje ya nchi kwa miezi 3 hapa hapa Africa, nyuma niliacha mke na watoto wawili walio primary school,
nikiwa kozi rafiki yangu akawa anakwenda kulala kwangu mara kwa mara especially weekends, akawa analala chumbani kwangu, haijajulikana hadi leo walianza lini uhusiano huo, alikua akienda kwangu kwa gia ya kuwaona wanaendeleaje.

Niliporudi, nikakuta wife kamtimua kazi house girl wetu bila maelezo ya kueleweka, nikapuuzia, baadae rafiki kipenzi wa wife wa tangu shule na ambae wanasali jumuia moja maana amepanga mitaa yetu, akaniambia kwa urefu uhusiano wa wife na mshikaji wangu, ila kwa sharti la kutomtaja whatsoever the case.

Baadae nikaona niende kumtafuta yule housegurl aliefukuzwa kazi na wife nikampata, aka confirm habari zile na kunieleza kwa kirefu na ndio kisa cha yy kufukuzwa kazi pale kwangu baada ya kumuhoji kuwa " kwanini unamfanyia shemeji matendo haya.

Baada ya kujiridhisha nikamuita wife mbele ya wazazi wake na kueleza kila kitu akabaki kimya akilia, nikamkabidhisha kwa wazee wake hapo hapo, akiwa kwao aliendelea kunibembeleza na kuniomba msamaha kwa kutuma watu mbali mbali wenye heshima, sikurudi nyuma, akasafiri kijijini kwetu kuwaona wazazi wangu na kuwaangukia, alikaa huko mwezi mzima.

Baadae wakaja wote na wazazi wangu hadi kwangu, wakasema pamoja na yote yaliyotokea niishi nae hivyo ametubu, sio ombi ni amri ndio maana wamemleta wao, moyoni nikasema najua cha kufanya, nilishindwa kuwaelewa, wanamtetea mtu ambae ameniumiza despite kuwa nilimuachia kadi ya benki awe anachukua mshahara wangu kuendesha familia, mimi kule kozi nikawa naishi kwa chakula cha kulipiwa na posho kidogo tu.

Wazazi walipoondoka tu, nikaanza kumfanyia visa na matendo mabaya ili aondoke, nikatafuta msichana wangu nikawa najiachia nae pale mtaani bila woga, nakunywa nae bar za mtaani, nikaanza kuja nae home nalala nae chumba kingine, akawa anatufanyia fujo lakini namdhibiti kiume hadi tunajifungia chumbani, nilikua nafanya haya yote ili wife aondoke lakini wapi, yupo tu, anawapigia simu wazazi kushitaki wakinipigia nawaambia huyu ni mke wenu mimi nilimtimua nyinyi mkamleta tena, ni mke wenu.

Tumeishi kwa hali hii tangu 2012 hadi sasa, yule msichana wangu akachoka hizi vurugu akaamua kuniacha, sasa nina mwingine, sina uhakika kama yupo mwanamke huko nje angeweza kuvumilia matendo niliyomtendea huyu wife, lengo ni aondoke lakini hataki kuondoka hata baada ya kumu offer kugawana mali, watoto wameathirika sana na hizi vurugu huwa nikiwapeleka kwa dada yangu wanakataa kurudi

Lakini yote haya aliyasababisha yeye kwa tamaa, nilishamueleza tangu siku ya ndoa kanisani kuwa nitakusamehe yote lakini uzinzi huwa sisamehi, sijamgusa tangu 2012.

Wadau naombeni ushauri nimtoe vipi huyu mwanamke?
Au mnadhani ipo siku naweza kusahau usaliti wake na kumpenda?

Na kama ni kumuacha ndani tutaishi hivi hadi lini?

Kuhusu watoto mnaonaje niwaache uko uko kwa dada yangu walelewe huko wasomee huko huko? Maana tangu likizo ya December wamekatalia huko hivyo school bus huwa linawafuata huko badala ya kwangu.

Nitaheshimu mawazo yenu as my last resort.
Mwisho wa uzinzi ni ndoa kuvunjwa. Hakuna kuishi na mtu mzinzi hata siku moja.
Yote nitavumilia lakini sio swala la uzinzi...
Ni kweli amekosea lakini hakuna duniani mwanamke asiyekosea, kosa lake huyu uliyafahamu makosa yake. Hata wakati wa Yesu wanawake walikuwa wakikosea sana na kushtakiwa kwa Yesu, lakini adhabu alizokuwa akitoa Yesu hakuna kama hiyo uliyoitoa kwa mke wako.

Ni heri ya kukaa na huyo mkeo ambae ameyatambua makosa yake kuliko kuoa mke mwingine ambae huna uhakika kesho atakukosea nini pia.

Kumbuka kuwa mwanamke hata wa bibilia ni mwepesi sana kudanganyika bila kujali ana pesa nyingi ama kidogo, hata huyo wako nadhani hukumkuta akiwa na bikra yake. kWAKUWA YAMEMKUTA HATATAKA KUMKUTA TENA NA AMBAYE HAYAJAMKUTA HAJUI UBAYA WA KUKUTWA NA KILICHOMKUTA MKEO. MSAMEHE MGANGE YAJAO, JALI WANAO NDIYO ZAWADI ILIYOKUBWA KUPITA ZOTE.
 
Wakuu habari zenu,

Mwaka 2012 nilienda kozi nje ya nchi kwa miezi 3 hapa hapa Africa, nyuma niliacha mke na watoto wawili walio primary school,
nikiwa kozi rafiki yangu akawa anakwenda kulala kwangu mara kwa mara especially weekends, akawa analala chumbani kwangu, haijajulikana hadi leo walianza lini uhusiano huo, alikua akienda kwangu kwa gia ya kuwaona wanaendeleaje.

Kuhusu watoto mnaonaje niwaache uko uko kwa dada yangu walelewe huko wasomee huko huko? Maana tangu likizo ya December wamekatalia huko hivyo school bus huwa linawafuata huko badala ya kwangu.

Nitaheshimu mawazo yenu as my last resort.
mkuu, pole sana, nakushauri kwa faida ya watoto wako, msamehe. hayo uliyomtendea yanatosha. tulieni ili mlee watoto na watoto waishi na saikolojia njema, wakikuwa wakuwe na akili njema, sio kama hizo zenu za ugomvi. itawaathiri sana watoto.

pia, unakaribisha magonjwa, mwanamke yeyote unayeenda kulala naye wakati akijua wewe una mke, huwa hakuthamini, hata kama ana virusi atakuambikiza tu kwasababu anajua wewe upo pale kumtumia tu ila si kumuoa au kumheshimu, anatumika kama chombo tu. kuna siku ukija kupata ngoma utatamani ungepata chance urudi nyuma utulie hata mkeo angechiti mara mia lakini usipate magonjwa, utawaacha watoto wako wawe yatima. usikie tu uyatima, sikia tu kwa mwingine. uwaangalie watoto wako, urudi.

pia mkiendelea hivyo, ujue mkeo naye ni binadamu, atakuja kukuua, au na yeye atatafuta kiserengeti pembeni, atakuwa anatoka nacho kwa siri kutimiza haja zake, ndo maana hata ukija na mwanamke yeye bado tu ana wewe kwasababu pengine anajua na yeye alishafanya. hayo ni mambo wanayofanya watoto wadogo si kwa watu wenye watoto hadi wawili kama ninyi, you have to grow up, babako na mamako wangetengana wewe ungekuwa na hali gani sasaivi? try to step into the shoes of your kids man! acha ujinga, pia kumbuka, usiposamehe na Mungu hatakusamehe, hii dunia inapita na mambo yake yote. usijidanganye. acha kiburi, msamehe, anzeni maisha mapya....labda kama ulimkuta bikra.

kwani wakati upo kwenye ndoa, wewe haujawahi kucheat? sema ukweli wako wote, mmezaa watoto wawili, haujawahi kucheat? acha upumbavu bro.
 
LUKE 17: 3 - 4 “If your brother or sister sins against you, rebuke them; and if they repent, forgive them.
4 Even if they sin against you seven times in a day and seven times come back to you saying ‘I repent,’ you must forgive them.”....FORGIVE...FORGIVE...FORGIVE!!
 
Unajua ndoa zina changamoto nyingi. Kuchapiwa mke kunauma sana. Pole sana

Hakuna mkamilifu chini jua. Tafakari kwa kina kabla hujafanya maamuzi mabaya.
Mkuu kuchapiwa mke tena na rafiki yako, hiyo inauma sana. kama alivyosema [TAG]msalala kwetu[/TAG]siwezi kusamehe maana hiyo ni dharau iliyo kubuhu. Mkuu watoto peleka shule, the hama hapo ulipo na kama nyumba ni yako ondoka na hati.[TAG]miss chagga[/TAG] kakupa ushauri mzuri sana.
 
Back
Top Bottom