Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Mama huyu ametoa malalamiko yake kuwa watu wazima wanasababish foleni kuwa ndefu. Waruhusiwe tu wenye watoto na wazazi au walezi wao.
Ameendelea kusema watoto wanaposikia njaa foleni za kununua chakula ni ndefu na wengi wao ni watu wazima wasio na watoto. Kuna mtoto wa miaka mitatu alikua wana njaa na alilia sana alipomuona bibi wa makamo ameshikilia pretzel 🥨 akitoka kuinunua.
Disney World wamemjibu mama huyu kuwa wakubwa ni watoto waliokua na wana uhuru wa kwenda Disney kama wengine wote.